Tanzania yawa mshindi wa tatu katika tuzo za taasisi zinazosimamia biashara duniani,2020

 

****************************************

Dar
es Salaam – Oktoba 14, 2020

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa mshindi wa Tatu kupata Tuzo za
Taasisi zinazosimamia Biashara Duniani, 2020 (WTPO Awards 2020) katika
kipengele cha matumizi bora ya ushirikiano (Best use of Patnership)
katika huduma ya kliniki ya Biashara inayosimamiwa na Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)


Tuzo
hizi zimetangazwa leo tarehe 14 Oktoba, 2020 jijini Geneva nchini
Uswidi ambapo Tanzania imewakilishwa na Mhe Balozi Maimuna Kibenga
Tarishi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika ofisi za Umoja wa
Mataifa- Geneva.


Tuzo
hizo zinazosimamiwa na kutolewa na Kituo cha Biashara cha Kimataifa
Duniani (ITC) ili kutambua michango ya Taasisi zinazosimamia sekta ya
biashara duniani (TPO) katika kusaidia Wafanyabiashara wadogo na kati
(SMEs) kuimarisha uzalishaji bora wa bidhaa zao, kuwajengea uwezo wa
kufanya biashara na kuweza kuuza bidhaa wanazozalisha nje ya nchi.


Kwa
mara ya kwanza Tanzania kupitia taasisi yake ya TanTrade imeweza
kushiriki tuzo hizo katika kipengele cha matumizi bora ya ushirikiano
kupitia huduma ya Kliniki ya Biashara kwa ushirikiano wa Benki ya
Biashara ya Tanzania (NBC) ambapo huduma hii inalenga kutatua changamoto
zinazowakabili wafanyabiashara Wadogo, wa Kati na Wakubwa nchini baada
ya serikali kuwa na andiko la Blue Print ili kujenga mazingira rafiki ya
ufanyaji biashara na kuweza kufikia uchumi wa viwanda.


Tangu
kuanzishwa kwake, huduma hii imepokea changamoto za wafanyabiashara
1,083 na kufanikiwa kutatua changamoto 229 na kero 705 zinashughulikiwa.
Huduma imeweza kutolewa kwenye Maonesho 17 yaliyoratibiwa katika mikoa
ya Dar es Salaam, Zanzibar, Pwani, Geita, Singida, Simiyu na Arusha


Mashindano
ya Tuzo hizo hutolewa kila baada ya miaka miwili ambapo Tanzania kwa
mara ya kwanza amekuwa mshindi wa Tatu akitanguliwa na Uswidi na Viet
Nam katika kipengele cha matumizi bora ya ushirikiano. Nchi nyingine
zilizoshiirki katika kundi hilo ni Colombia, Misri, Uholanzi, na
Zimbabwe ambazo ziliingia kwenye kwenye mchujo wa mwisho.