Wana ccm kata ya osunyai wapewa somo



Diwani mteule kata ya Olasiti, Christopher Salvatory 


Na Mwandishi wetu Arusha

WANACHAMA wa
Chama Cha Mapinduzi kata ya osunyai jijini hapa wametakiwa kutekeleza kwa
vitendo ahadi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na chama hicho lakini pia
kumuunga mkono Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa njia ya utekelezaji wa ahadi
hizo.

Kwa sasa Chama Cha Mapinduzi hususani kwa mkoa wa Arusha
kimefanikiwa kutekeleza ahadi mbalimbali zilizotolewa na Chama cha mapinduzi
katika ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2015 ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya,
barabara, maji na kuwawezesha wananchi wa Arusha kiuchumi.

Akizungumza na wananchi wa kata hiyo, Christopher
Salvatory  ambaye ni mgombea mteule wa udiwani kata ya Osunyai jijini
Arusha alisema katika kuelekea uchaguzi mkuu, CCM itatoa ilani yake ambayo kila
mteule atapaswa kuifuata na hivyo kutoa wito kwa kila mwana CCM kutekeleza
ilani hiyo itakapozinduliwa rasmi wakati wa kampeni.

Amefafanua kuwa kwa kupitia nuru na uwajibikaji wa Raisi ,Magufuli
ni wazi kuwa kila mgombea ambaye anawakilisha chama cha mapinduzi anatakiwa kuwa
mfano na kuahidi kuwa yeye atakapochaguliwa kuwa Diwani atatekeleza ilani ya
CCM.

” Rais wetu ameonesha uzalendo mkubwa sana na sisi kama
wadau tunatakiwa kuhakikisha tunamuunga mkono kwa kuonyesha  uwajibikaji na usimamizi wa miradi mbalimbali
na hii itasaidia kuondolewa kwa na changamoto lukuki ambazo bado zinawakabili
wananchi wetu,”aliongeza

Katika hatua
nyingine mgombea huyo alisema kuwa CCM imempa heshima kubwa sana ya kuweza
kupeperusha bendera ya kata hiyo ya Osunyai lakini pia ana mpango wa
kuhakikisha kuwa anatatua changamoto zikiwemo za miundombinu imara ndani ya
kata hiyo

Alihitimisha
kwa kuwataka wana CCM kuwa kitu kimoja na kuweza kutafuta kura kwa kishindo za
wagombea kuanzia ngazi ya udiwani na Urais.