Mahakama kuu Tanzania kanda ya Kigoma imewaachia huru washtakiwa 11 wa kosa la mauaji ya askari wawili wa jeshi la polisi yaliyotokea kwenye mapigano baina ya wananchi na jeshi hilo mwaka 2018 katika eneo la Mpeta wilayani Uvinza baada ya ushaidi uliowasilishwa kupingana.
Kesi namba 2 ya mwaka 2020 makosa mawili ya kuuwa kwa kukusudia askari wa jeshi la polisi Inspector Ramadhan mdimu na Copro Mohamed Nzengo tukio lililotokea mwaka 2018 mwezi wa 10 iliyosimamiwa na mawakili wa serikali Happyness Mayungu,Shaban Masanja na Riziki Matitu huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na wakili Sadik Aliki,Kagashe Rweyumamu na Eliuta Kiviylo
Akisoma maelezo ya mwenendo wa kesi hiyo jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Kigoma Ilvin Mgeta amesema ushahidi uliotiliwa shaka ni maelezo ya washtakiwa kupigwa risasi kwenye mapambano yao na askari wakishambuliana uso kwa uso wakati majeraha yanaonyesha walipigwa risasi kwa nyuma na kutokea mbele ,ushahidi wa daktariwa kituo cha afya cha Lugufu alioutoa mahakamani kuwa hawakupigwa risasi bali zilipita juu ya ngozi wakati makovu yakiwa yanaonyesha risasai kupita upande mmoja na kutokea wa pili hivyo mahakama kueleza kushangazwa na nia ya shahidi huo kuipotosha mahakama.
Gwaride la utambuzi ambalo halikukidhi matakwa ya sheria kwani washtakiwa waliwekwa kwenye mstari wakati wakiwa peku na wakiwa na majaraha ya risasi huku nguo zikiwa zimejaa damu hivyo kurahisisha kutambuliwa ,ushahidi wa askari aliyeeleza kushuhudia askari mwenzake akiuuawa na mazingira ya kukamatwa kwa washtakiwa kwani kila mmoja alikamatwa maeneo tofauti ,ushahidi wa maelezo ya onyo ambayo washtakiwa waliyakana mahakamani kuwa hawakuandika wao na shadidi mwingine wa gwaride kuiambia mahakama kuwa hakuonana na washtakiwa hao kwenye utambuzi
Jaji Mgeta amesema kutokana na utata huo ushahidi wote ni dhaifu na hauwezi kuwaweka hatiani washtakiwa hivyo washatakiwa wote 11 wako huru.