na Wananchi mara baada ya treni hiyo ya mizigo ikiwa na mabehewa 10
yenye tano 400 kuwasili katika stesheni ya Arusha mapema leo saa tano
ikiwa ni safari ya majaribio kabla ya usafiri huo kuanza mwezi huu
mwishoni picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha
Sehemu ya wananchi wakiingalia Treni mara
baada ya kuwasili kwenye Stesheni ya Treni Jijini Arusha ikiwa ni
safari ya kwanza baada ya miaka 34 iliyopita kusimama kwa usafiri huo
jijini hapa
Wananchi waliofika kuipokea Treni ya mizigo ya
majaribio kwenye hafla ya mapokezi leo jijini Arusha kama walivyokutwa
na kamera ya matukio jijini Arusha wakiilaki treni hiyo ikiwasili
kwenye Stesheni ya Railway iliyopo Krokoni Kata ya Levolosi jijini
Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha
Wananchi wakifuatlia hotuba ya Katibu wa chama cha
Mapinduzi wilaya ya Arusha Mwita Zakaria kwenye hafla ya mapokezi ya
Treni ya mizgo iliyowasili leo ikiwa ni safari yake ya kwanza baada ya
miaka 34 kupita na kuanza tena kutoka huduma mwishoni mwa mwezi
huu.
Sehemu ya Mabehewa kumi ya Treni hiyo ya
mizigo kama yalivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha mapema leo
katika Stesheni ya Reli iliyopo eneo la Krokoni kata ya Levolosi
jijini Arusha
Baadhi ya wananchi wakipata fursa ya kupiga picha na
usafiri huo wa Treni ikiwa ni sehemu ya hafla hiyo mara baada ya
kuwasili katika stesheni ya reli iliyopo kata ya Levolosi jijini
Arusha
Umati wa wananchi na wakazi wa jiji la
Arusha waliojitokeza kwenye hafla ya kuwasili kwa treni ya mizigo
iliyowasili kwa mara ya kwanza baada ya kitambo kirefu kusimama kwa
usafiri huo takribani miaka 34 iliyopita usafiri huo utaanza rasmi
mwishoni mwa mwezi huu.
Na Ahmed Mahmoud Arusha
MAMIA ya wananchi jijini Arusha wamejitokeza kwa
wingi
kwenye hafla ya mapokezi ya Treni ya mizigo ya majaribio iliyowasili ikitokea
Dar es salaam na mabehewa kumi ya Saruji yenye tani 400 na kupokelewa na Mkuu
wa wilaya ya Arusha.
Akizindua hafla hiyo ya
mapokezi ,mkuu wa wilaya ya Arusha,
Kenani Kihongosi, amewaomba wananchi kuhakikisha wanailinda na kuitunza miundo
mibinu ya reli ili iweze kudumu na kuwahudumia wananchi .
Ametoa wito kwa wafanyabiashara kuitumia treni
hiyo ya
mizigo kusafirishia bidhaa zao
na hivyo kuwapa unafuu wa bei ya bidhaa na kuboresha maisha ya wananchi kama
lilivyo lengo la serikali ya awamu ya Tano kuinua maisha ya
watanzania.
Alisema kuwa
ujio wa treni hiyo ya Mizigo ni mwanzo wa treni nyingine ikiwemo treni ya
Abiria itakayosaidia kusafirisha na kushuka kwa bei za bidhaa ikiwemo saruji na
usafiri wa Abiria kwa bei ya 18,000 badala ya elfu 30,000 hadi 35,000 kwa
usafiri wa mabasi.
Aidha
alisema
kuwa treni moja itakuwa inapakia tani zaidi ya mia nane za Mizigo sawa na
malori 80 na hivyo kusaidia kuokoa uharibifu wa barabara unaosababishwa na
wingi wa malori ya Mizigo
“Wananchi
lindeni na kutunza miundombinu ya Reli ili isihujumiwe na kuturudisha katika
zama za kale jambo ambalo tunatakiwa tuliona na kutoa taarifa kwa haraka katika
kudhibiti matukio kama hayo”alisema Mkuu huyo
Awali mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro
aliyewasili na treni hiyo kutokea kituo cha Usariver wilayani Arumeru, hadi
jijini Arusha alisema kwa mara ya kwanza treni hiyo ya mizigo
inatambulishwa rasmi kwa wananchi na huo ni mwanzo wa safari ya
maendeleo na kuashiria kupokelewa kwa treni ya abiria ambayo itaanza mwishoni
mwa mwezi huu wa Augosti 2020.
Alisema
serikali ya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa
na daktari John Magufuli, inatekeleza Ilani ya uchaguzi kwa vitendo na sio
maneno na wananchi ni mashahidi.
Muro,
amewaomba wafanyabiashara kuituma fursa hiyo ya
uwepo wa treni hiyo kusafirisha bidhaa za viwandani kutoka mikoa mbalimbali
kuipeleka mkoani Arusha kutoka na kwenda mikoa mingine.
Akitoa salamu zake ,Katibu wa Chama cha
Mapinduzi,wilaya ya
Arusha, Denis Mwita, amesema ujio wa treni hiyo ni kurahisisha huduma ya
usafirishaji wa mizigo na kuwapunguzia gharama za mizigo na
usafirishaji wananchi.
Alisema sasa Chama cha
Mapinduzi kimefikia mwishoni mwa
utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020 ambayo imetekelezwa
kwa vitendo na wananchi ni mashahidi kwa maendeleo yaliyopatikana katika
kipindi cha miaka mitano ya awamu ya kwanza ya rais Magufuli.
Katibu mwita, alisema mkoa wa Arusha, una viwanda
vingi
ikiwemo vya mabati na chuma lakini ni mkoa ambao hauna kiwanda cha Saruji
hivyo treni hiyo itatumika kusafirishia pia Saruji kutoka kwenye mikoa
mingine inakozalishwa na kuileta Arusha hivyo kupunguza gharama za
bei za bidhaa na kuwataka wananchi kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi na
serikali yake.
Aliwaambia wananchi kwamba
hawana cha kumlipa rais Magufuli,
kutokana na aliyoyafanya hivyo wahakikishe wanamlipa kwa kumpatia kura za
kutosha kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.
Baadhi ya wananchi waliokuwepo kwenye hafla hiyo
wameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuwasogezea huduma hiyo ya usafiri
na kuwapunguzia gharama za nauli kutoka kiasi cha 30.000 hadi Elfu
kumi na nane