Wakulima, wafugaji washauriwa kuwa karibu na wanasheria

 Na Queen Lema, Arusha

Wakulima na wafugaji wameshauriwa kutumia vyombo mbalimbali vya sheria katika shughuli zao za kila siku ili kujiepusha na madhara yanayowakumba kila wakati na kuwasababishia hasara kubwa.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Asasi ya Smart Community on legal Organization, Bi Mary Mwita mapema jana wakati akiongea na waandishi wa habari,wakulima na wafugaji,ambao walitembelea banda la asasi hiyo kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji (nane nane) yanaondelea katika viwanja vya Themi Arusha

Mwita alisema kuwa kwa sasa wakulima pamoja na wafugaji hawana elimu ya kutosha juu ya haki zao hali ambayo wakati mwingine inawasababishia hasara kubwa sana

Aliongeza kuwa wakulima na wafugaji wanapata hasara na wakati mwingine wanapoteza ushahidi wao wenyewe kwa kutojua wanachotakiwa kukifanya wakati wa kununua bidhaa

“Hapa tunakutana na makund

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kanani Kihongosi akiwa katika banda la Smart Community, na pembeni yake ni Mkurugenzi wa asasi hiyo Mwanasheria Mary Mwita
Naibu Waziri wa Kilimo akisalimia na mkurugenzi wa Smart Community Mary Mwita alipotembelea banda hilo katika viwanja vya nane nane jijini Arusha 

i haya mawili wengi wameonesha sana kuingia hasara kutokana na kununua bidhaa feki ambazo hazina matokeo sasa wanabaki wakiwa wanalalamika tu hapo hata tukitaka kuingilia kati hatuwezi kwa sababu mara nyingine hawana hata vielelezo vinavyotakiwa” aliongeza

Alisema kuwa ili makundi hayo mawili yasiteseke tena wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanahifadhi vielelezo vyote vya kununulia vifaa na madawa ambapo kama shida itatokea basi itakuwa ni raisi sana kuweza kusaidiwa kwa mujibu wa sheria

Nawasihi sana hata wanunuzi wa pembejeo za kilimo ambao mara nyingi wanawauzia wakulima wahakikishe kuwa wanaingia mikataba wasifanye kazi kiholela holela hio itawasaidia kupata haki zao za kisheria hasa pale watakapokuwa na matatizo mbalimbali”aliongeza

Alihitimisha kwa kuwataka wakulima na wafugaji kuhakikisha kuwa wanatumia vyema kituo hicho kwa ajili ya kupata elimu muhimu juu ya haki zao ambapo itawalinda dhidi ya uonevu wa aina yoyote ile.