Wakati Taifa likielekea kwenye Uchaguzi Mkuu Mwezi Oktoba 2020, Mkuu wa utumishi Jeshini Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli amewatahadharisha Askari wa Jeshi la wananchi kujihadhari na ushabiki wa Kisiasa
Meja Jenerali Simuli ametoa tahadhari hiyo wilayani arumeru Mkoani Arusha katika kikosi cha Jeshi 833 Oljoro, Wakati wa kufunga mafunzo ya askari wapya kundi maalumu la nne la mwaka 2020 mchepuo wa sayansi, ambapo wakiwa katika mafunzo, Askari hao wapya walipitia mafunzo mbalimbali ya kijeshi ikiwemo ujasiri na matumizi ya silaha nzitoo za kivita.
Meja Jenerali Simuli amesema kwa kufanya hivyo wanaweza kuhatarisha amani ya taifa, huku akiongeza kuwa Askari hao bado wanao Uhuru wa kumchagua kiongozi wanaye mtaka kama walivyo raia wengine.
Naye Mkuu wa Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi, RTS Kihangaiko Canali Sijaona Myala, ameliomba Jeshi kuendelea na mkakati wake wa kutoa mafunzo hususani kwa vijana wasomi ili kupata Jeshi imara la wasomi.
Zaidi ya Askari wapya 400 kundi maalumu la nne la mwaka 2020 mchepuo wa Sayansi wamehitimu mafunzo hayo