Rc.gambo,wadau shirikianeni na serikali mapambano dhidi ya covid 19

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akipokea Vitakasa mikono lita 2500 pamoja na Ndoo 50 kutoka kwa meneja wa kampuni ya Mega beverages Christopher Ndossi  leo jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.

Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega akitoa taarifa ya mapambano ya ugonjwa wa Covid 19 kwa mkoa wa Arusha kwa wadau kutoka kampuni za Hanspoul Ltd,Simba Truck na Mega Beverages Mara baada ya kukabidhiwa vifaa na fedha milioni 29 kutoka kwa wadau hao ikiwa ni sehemu yamsaada dhidi ya mapambano vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona Leo jijini Arusha.

Mkuu wa mkoa wa Arusha akitoa sehemu ya msaada wa vitakasa mikono na ndoo kwa ajili ya Magereza ya mkoa wa Arusha kwa kamanda wa jeshi hilo mkoani hapa leo leo kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha

Mkuu wa mkoa wa Arusha akiongea Mara baada ya kupokea msaada wa vifaa vya kujikinga na maandalizi ya ugonjwa wa Covid 19 kutoka kampuni za Hanspoul Ltd,Simba Truck na Mega Beverages zote za jijini Arusha kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha

Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Koka Moita akipokea sehemu ya vitakasa mikono na ndoo kwa ajili ya mahabusu kwenye vituo vya Muriet Kikuu vya jijini hapa ikiwa ni sehemu ya msaada wa mapambano ya ugonjwa wa Covid 19.
Mkurugenzi wa kampuni ya Hanspoul Saitbir akiongea Mara baada ya kukabidhi hundi ya milioni kumi akiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona Leo jijini Arusha
Kaim kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Koka Moita akiongea kushukuru Mara baada ya kupokea msaada huo leo jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha

Meneja wa kampuni ya Mega Beverages Christopher Ndossi akiwa na kamanda wa Magereza Mkoa wa Arusha sanjari Mkuu wa mkoa wa Arusha Mara baada ya makabidhiano hayo ya Ndoo 50 na lita 2500 ya vikatasa mikono Leo jijini Arusha.

Na Ahmed Mahmoud Arusha

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amepokea lita 2500 za vitakasa mikono na ndoo 50 za kuoshea mikono Sanjari na hundi za fedha ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid 19.
Kwa muktadha huo  ameendelea kuwataka wananchi kuendelea kuchukuwa hatua za kudhibiti Ugonjwa wa Covid 19 kwa kufuta maelekezo na kuacha misongamano isiyo ya lazima.
Akiongea wakati wa Makabidhiano hayo kutoka kampuni za Mega Beverages Hanspaul na Simba Truck Gambo alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuendelea kuchukuwa hatua zaidi za kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo zinazoelekezwa na Serikali 
Alisema kuwa kila mmoja wetu tuache kukusanyika kwenye maeneo yenye misongamano isiyo ya lazima na kuwataka wenye mabasi daladala kuacha kujaza na kuendelea kuchukuwa hatua kwa kuweka maji tiririka vituoni.
“Kama Serikali tunawashukuru Sana wadau hawa ambao wameonyesha kushirikiana nasi katika kukabiliana na janga hili la Ugonjwa wa Covid 19 nasi tutaendelea kuchukua hatua zaidi za kukabiliana na ugonjwa huu”
Alisema kuwa wananchi tusijiamini Sana kwa kuwa Ugonjwa huo unaua kwa kuepuka misongamano isiyo ya lazima na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Serikali huku akibainisha kuwa wanahitaji kiasi cha milioni 196 za ukarabati wa eneo la wagonjwa kama walivyoelekezwa na Waziri wa Afya na shirika la Afya Ila la awali limekamilika.
Awali Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega alisema kuwa tangia tukio la kwanza kutangazwa wamekuwa wakishirikiana na wadau jinsi ya kupata vifaa sanjari na utoaji wa elimu ikiwemo ushiriki wa juu ya mapambano ya Covid 19.
Alisema kuwa kumekuwa na mahitaji mengi ya vifaa ndani ya jamii yetu na kama Serikali imeendelea kushirikiana na wadau mbali mbali kuona jinsi ya kusaidiana kupata vifaa kuisaidia jamii.
Kwa Upande wao Meneja wa Mega Beverages Christopher Ndossi na Mkurugenzi wa Hanspoul na Mkurugenzi wa Simba Truck wamesema kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wanaendeleza kupambana  Ugonjwa huo na huo ni mwanzo wa msaada huo.