Ufaransa yaongeza mwezi mmoja wa tahadhari dhidi ya corona

Ufaransa imeongeza muda wa kuendelea kuchukua tahadhari za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona hadi Mei 11. 


Rais Emmanuel Macron amesema ifikapo tarehe hiyo shule zitaanza kufunguliwa. 

Jumatatu
Ufaransa imeripoti vifo 574 vinavyotokana na maambukizi ya virusi
hivyo, na kuifanya idadi jumla ya vifo kufikia watu15,000. 

Hata hivyo, idadi ya wagonjwa wa COVID-19 wanaohitaji uangalizi maalumu imepungua kwa siku ya tano mfululizo. 

Macron
amesema kasi ya janga hilo inaanza kupungua na dalili za kudhihirisha
hilo ziko wazi. “Mei 11 itakuwa mwanzo wa awamu mpya. Sheria zinaweza
kubadilishwa kulingana na hali itakavyokuwa,” aliongeza Macron.

Serikali
mbalimbali kote ulimwenguni ziko chini ya shinikizo la kuokoa uchumi wa
dunia usije kuanguka kabisa kwa sababu ya kufungwa kwa biashara na watu
kulazimika kubakia majumbani, lakini viongozi pia wanajaribu kuzuia
wimbi la pili la ugonjwa huo.