Wananchi wa Kijiweni Iringa wakiwa amebeba mwili wa marehemu Raymond Mdota aliyeuwawa
Nguo za marehemu zikiwepo eneo ambalo mauwaji yaliyofanyika
Askari polisi wakitoka eneo ambalo mwili ulitupwa
Umati wa wananchi ukiwa eneo la tukio bila tahadhari ya virusi vya Corona
Eneo la klabu cha kijiweni ambako mauwaji yaliyofanyika
Mwili wa Raymond Mdota ukiwa umetupwa kwenye shamba la mahindi
……………………………..
Na Francis Godwin, Iringa
MAUAJI ya kinyama yamefanyika usiku wa ijumaa kuu Iringa eneo la Kijiweni kata ya Kwakilosa katika Manispaa ya Iringa baada ya mhubiri wa injili na mgombea ubunge mtarajiwa katika jimbo la Kalenga Raymond Mdota (46) kuuwawa kwa kuchinjwa shingo yake akiwa katika huduma ya kuhubiri injili kwenye klabu cha Pombe za kienyeji na mwili wake kutupwa kwenye mahindi.
Mashuhuda wa tukio hilo waliozungumza na mwandishi wa habari hizi eneo la tukio walisema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa Ijumaa na nje ya chumba kimoja wapo cha klabu cha pombe za kienyeji kijulikanacho kwa jila la Kijiweni Klabu .
Walisema kuwa kabla ya mauwaji hayo Mdota ambae ni mmoja kati ya walimu wastaafu alifika katika eneo hilo la Klabu cha Kijiweni akiwa na radio yake kubwa aliyokuwa akiitokota huku ikiwa inapiga nyimbo za dini na kuanza kuzunguka chumba kimoja hadi baada ya kingine akipiga muziki wa dini ya kikristo kwa ajili ya kuomboleza mateso ya Yesu Kristo na nyingine za kufufuka kwa Yesu .
“ Yaania alifika hapa mida kama ya saa mbili usiku akiwa na radio yake kubwa akipiga nyimbo za dini kwa sauti kubwa huku akicheza kwa fuhara na kuwasisitiza watu kuachana na dhambi na kumgeukia Mungu tulimfurahia sana hasa ukizingatia ilikuwa ni ijumaa kuu ya mateso ya Yesu ila muda ulipozidi kusogea katika radio hiyo hiyo alianza kupiga nyimbo za muzidi wa kidunia na kuanza kutangaza siasa kuwa yeye ni mkazi wa Magumbike na anampango wa kwenda kugombea ubunge wa jimbo la kalenga “ alisema mmoja kati ya mashuhuda ambae hakutaka kutaja jina lake.
Alisema wakati akihubiri injili alikuwa ameshika rozari yake mkononi ila baadae alipokuwa akitangaza siasa alishika skafu yenye rangi ya bendera ya Taifa huku akisisitiza kuwa yeye ndie mbunge mpya wa kalenga bila kutaja kupitia chama gani na wakati huo akinywa pombe aina ya Ulanzi na kuwanunulia watu pombe huku akicheza muziki .
Hata hivyo alisema wakati muda wa kufunga klabu hicho ukielekea kufika wao waliondoka na kumwacha yeye na watu wachache wakiendelea kuwepo kwenye vyumba vichache ambavyo vilikuwa havijafungwa eneo hilo kabla ya asubuhi kuambia tukio hilo la kuuwawa kwake .
Johari Ngeng’ena mjumbe wa serikali ya mtaa wa Kijiweni alisema kuwa mauwaji hayo ni ya kwanza kwa mwaka huu na kuwa ila tukio hilo ni la kinyama zaidi na limewasikitisha wananchi wa mtaa huo .
Hata hivyo alisema kuwa kutokana na tuko hilo wanampango wa kukaa nchini ili kuangalia uwezekano wa kuanzisha ulinzi wa jadi (sungusungu) pia kuwataka wafanyabiara wa pombe katika eneo hilo kuwa na muda mzuri wa kufunga na wale waliolima mahindi mitaani basi kupewa taratibu za manispaa za kuacha kulima mahindi mitaani kwani mwili wa marehemu huyo umetupwa kwenye mahindi .
Beth Mdeta ambae ni muuzaji wa chumba ambacho nje mauwaji hayo yalifanyika alisema kuwa kwa upande wake alifunga mapema na kumuacha Mdota akiwa kwenye katika maeneo ya klabu hicho na sio ndani ya chumba chake na kuwa amesikitishwa na kusikia mauwaji hayo yamefayika nje ya chumba chake .
“ Mimi nilipigiwa simu asubuhi na majirani zangu wakinieleza kuwa nje ya chumba change kuna mauwaji yamefanyika maana kuna damu nyingi na baadhi ya vitu kama mabaki ya nguo yakiwa yametelekezwa nje eneo lenye damu nyingi “
Mwenyekiti wa Klabu hicho Nicolina Mapunda alisema kwa upande wake marehemu hamfahamu kabisa na hata huo usiku ambao watu wanadai walimuona eneo hilo kwa upande wake hakubahatika kukutana nae zaidi ya kupigiwa simu majira ya saa 2 asubuhi .
Alisema kuwa yeye amekuwa akifanya kazi ndani ya klabu hicho na wafanyabiashara wenzake walimwita na kumuonesha damu zilizotapakaa eneo hilo japo alisema utaratibu wa klabu hicho kufungwa ni saa 5 usiku ila siku hiyo yeye aliondoka mapema zaidi .
Mwili wa marehemu huyo ulikutwa ukiwa umechinjwa shingo na kitu chenye ncha kali huku viatu vyake pamoja na radio yake vikiwa vimeporwa na wauwaji hao na mifuko ya suruali ikiwa nje kwa maana ya pesa alizokuwa nazo kusachiwa na wauwaji hao huku mkononi akiwa ameshikilia rozari yake.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Juma Bwire amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kuwa lilitokea majira ya saa10;20 alfajiri na kuwa jeshi la polisi linaendelea kuwasaka watuhumiwa wa mauwaji hayo