Wadau kigoma waungana kutoa taulo za kike kwa wanafunzi sekondari ya mkulima ….

Uongozi wa inspirational women Group na wanachama wake wakiwa wameshika taulo za kike kabla ya kuwakabidhi wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mkulima
Mwenyekiti wa Inspirational women Group akitoa mada ya hedhi salama kwa wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari ya Wakulima iliyopo katika Manispaa ya Kigoma ujiji.

ASASI isiyo ya kiserikali ya Inspirational women Group  na shirika la msalaba mwekundu Tanzania (red  Cross) na  wadau mbalimbali   Kigoma wamesaidia wanafunzi wa kike 150 wa sekondari ya Wakulima Kigoma ujiji  mkoani Kigoma  msaada wa Taylor za kike .mwandishi Editha Karlo anaripoti kutoka Kigoma

Mwenyekiti wa women inspirational Aisha John kabla ya kugawa taulo hizo alisema kuwa mtoto wa kike anapokuwa kwenye hedhi anatakiwa awe na amani  muda wote na waweze pia kusoma kwa utulivu na kujiamini.

Alisema suala la hedhi kwa mtoto wa kike ni suala la kawaida na si jambo la aibu au laana bali ni hatua za ukuaji za kimwili.

“Sisi wanawake tunajivunia sana tunapoingia hedhi kwani tunakuwa na uhakika tunaweza kubeba mimba na kuzaa mtoto hivyo suala la hedhi siyo la aibu au laana”alisema

Pia aliwataka wanafunzi hao wanapoingia kwenye hedhi kuzingatia usafi kwa  kuzifua taulo hizo kabla ya kuzitumia kwa mara nyingine.

Alisema kuwa ikiwa sasa hivi dunia inaelekea katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo hufanyi tarehe 8 mwezi wa tatu na mwaka huu Kitaifa inafanyika Simiyu na ujumbe wake ni “kizazi cha usawa kwa maendeleo ya Tanzania ya sasa na baadae”wameamua kusherekea siku hiyo na wanafunzi wa kike kwa kuwapatia taulo hizo ili wanapokuwa kwenye hedhi wasijisikie wanyonge.

Alisema katika kampeni hii  ya kuhamasisha hedhi salama kwa mtoto wa kike ni endelevu na itadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja  wamechagua shule tatu za sekondari kuanza nazo kwenye mpango huo ambazo ni Buteko Sekondari,Buhanda sekondari na Wakulima sekondari.

Mratibu wa chama cha msalaba mwekundu Tanzania kwa Mkoa wa Kigoma(red cross)Khalid Selemani Ausii akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi taulo za kike kwa wanafunzi hao alisema kuwa mtoto wa kike anapokuwa kwenye hedhi anatakiwa awe na amani na uhuru muda muda wote na wao kama chama wapo tayari kushirikiana na jamii katika mambo mbalimbali.

Alisema watoto wakike wanapokuwa kwenye hedhi zao wanatakiwa wasijisikie wanyonge kwa kukosa taulo za kike na kushindwa kuhudhuria masomo yao kwa ukamilifu.

Mkuu wa shule ya sekondari ya Wakulima William Siumbe Diara aliwashukuru insparation women Group pamoja na wadau walioshiriki kuwasadia watoto wa kike shuleni hapo kwa kuwapatia taulo za kike kutawafanya kusoma kwa kujiamini.

“Mmefanya jambo zuri salama tunawashukuru tunaomba hiki kitu kiwe endelevu kwani itawasaidia wanafunzi wa kike kuwa na uhakika wa masomo hata wanapokuwa kwenye hedhi na kuacha tabia ya kushindwa kuja shule sababu ya hedhi”alisema

Alisema msaada huo wa taulo za kike umekuja wakati muafaka na niwamaana kubwa na taulo hizo ndo zinafaa kulingana na mazingira kwakuwa mahudhurio ya shule kwa kila mwezi kwa watoto wa kike yanakuwa siyo mazuri kwasababu ya kushindwa kumudu gharama za taulo wanapokuwa kwenye hedhi.

Mwalimu mkuu huyo alisema shule yake inachangamoto ya upungufu mkubwa wa waalimu wa kike hali inayofanya waalimu wa kiume kusaidia kutoa huduma kwa watoto wa kike.

“Shuleni hapa tuna jumla ya waalimu 18 ambapo kati ya hao mwalimu wa kike ni mmoja tu lakini taarifa hii nimeshaiwakilisha kwa mwajiri wangu ambaye amehaidi kulifanyia kazi jambo hili”alisema

Aliitaja sababu kubwa inayochangia shule hiyo kukosa waalimu wa kike ni umbali wa kutoka stand ya magari na kufika shuleni.

“Hapa hatuna nyumbani za waalimu,kumpata mwalimu wa kike kila siku atembee umbali unaotumia dakika 30 hadi kufika hapa ni kazi ila mwajiri wangu analifanyia kazi suala hili”alisema

Mwanafunzi Imaculate Maico wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya wakulima anasema wamekuwa wanakutana na changamoto wanapo kuwa kwenye hedhi huwalazimu kurudi nyumbani huku masomo yanakuwa yanawapita.

“Tunajisikia wanyonge tunapoingia kwenye hedhi na kukosa taulo za kike,ila sasa hivi hali itakuwa tofauti baada ya  kupewa zile mada juu ya hedhi salama pamoja na kupewa taulo hizi tutajiamini na kuuhudhuria masomo kikamilifu”alisema
MWISHO