Tcra.ccc:vijana ndiyo wahanga wakubwa wa mitandao ya kijamii

Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari ya Arusha Day wakiwa wamekusanyika tayari kwa
kuwasikiliza Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za Mawasiliano
Tanzania TCRA.CCC walipotembelea shuleni hapo kuwapa Elimu.
Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari ya Arusha Day wakifuatilia kwa makini kile
kinachoelezwa na Baraza la Ushauri wa Huduma za Mawasiliano Tanzania
TCRA .CCC
Afisa Uhamasishaji kutoka Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania(TCRA.CCC)Hillary Tesha. 





Mary Shao Katibu
wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania
(TCRA.CCC)akizungumza na ana wanafunzi wa Shule ya Sekondari Arusha Day
Jan Kaaya Mhandisi Msaidizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA)akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Arusha Day.
Wakwanza kushoto ni Mhandisi mwandamizi TCRA kanda ya Kaskazini akiwa na baadhi ya wajumbe wa bodi Baraza la ushauri lawatumiaji wa huduma za Mawasiliano Tanzania(TCRA.CCC 
Happyness Kaaya mmoja wa mjumbe wa Baraza
la ushauri lawatumiaji wa huduma za Mawasiliano Tanzania(TCRA.CCC
)ambae pia ni mwalimu katika shule ya sekondari ya Arusha Day
Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari ya Arusha Day wakiwa wamekusanyika tayari kwa
kuwasikiliza Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za Mawasiliano
Tanzania TCRA .CCC walipotembelea shuleni hapo kuwapa Elimu.


Na.Vero Ignatus,Arusha.
 Baraza
la ushauri la watumiaji wa Huduma za Mawasiliano   Tanzania(TCRA.CCC
)limetoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Arusha Day kuhusiana
na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii,huduma za Mawasiliano,pamoja
na kuchukua maoni kutoka kwa watumiaji wa huduma hizo.

Akizungumza Afisa Uhamasishaji kutoka TCRA.CCC Hillary Tesha amesema
kuwa vijana ndiyo wahanga wakubwa wa mitandao ya kijamii na wakiachwa
bila kupewa elimu taifa litaishia kuwa na kizazi ambacho hakiheshimu
haki za binadamu,pia watakuwa wanatumia njia hizo za mawasiliano kwa
njia mbazo hazina msaada katika Maisha yao na litakuwa kama janga kwa
upande wao.

‘’Tumefanya
leo katika shule ya sekondari ya Arusha Day,tunampango wa kuelekea tena
shulre ya sekondari ya Kikwe na chou cha Ualimu cha Patandi’’Alisema
Tesha

Hadi
sasa TCRA-CCC limeshatoa elimu katika mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza
Lindi Mtwara Arusha lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa matumizi sahihi ya
za mitandao zinawafukia vijana wengi zaidi ili kuweze kuokoa vijana
katika matumizi ambayo siyo sahihi ya mitandao ya kijamii.

Katika
mkoa wa Arusha waliweza kukutana na kikundi cha waklemavu wameweza
kushauriana nao na kuchukua maoni na mambo mbalimbali wanayoweza
kuyatumia katika kuboresha huduma za mawasiliano katika mkoa na Nchini
kwa ujumla

Kwa upande wake Katibu wa Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano Tanzania Mary Shao aliwataka
wanafunzi hao kutumia mitandao ya kijamii kwaajili ya manufaa yao
wenyewe kama vile kujisomea na kujiimarisha kielimu Zaidi

‘’Wazazi
wenu pamoja na walimu wenu wanajisikia vibaya sana kutokana na matendo
nmayoyafanya huko mitaani kwenu,tulieni someni kwa bidii ili muweze kuja
kuwa na Maisha bora hapo baadae yasiyokuwa ya aibu’’Alisema Mary

Amewataka
kufahamu  kwamba zipo sharia zinazosimamia huduma hizo hivyo wasipokuwa
makini wanaweza wakajiingiza kwenye matatizo yatakayoleta aibu katika
Maisha yao

Amewasisitiza
kuepuka kuweka picha za hovyo (nusu uchi)kwenye mitandao ya kijamii ni
kujidhalilisha na kuondoa utu wao,hivyo basi mtumiaji wa huduma yeyote
ana wajibu wa kutumia huduma kwa kufuata sharia za nchi

”Nani
ajuae kwamba huko baadae  wanaweza kuja kuwa viongozi na taarifa zao
zote zikawa wazi  bila kificho,usikubali kujilaumu baadae’’Alisema Mary