Ukatili dhidi ya wanawake na watoto waanza kupatiwa ufumbuzi

Na Ahmed Mahmoud,Arusha

Tatizo
la Ukatili  dhidi ya   wanawake na watoto miongoni mwa jamii huenda
likapatiwa ufumbuzi wa kudumu baada ya wizara ya katiba na sheria
kuanza kuwapatia elimu viongozi wa dini na kimila ili waweze kuielimisha
jamii kuhusu haki ya mwanamke na watoto.

Akiongea
jijini Arusha naibu katibu Mkuu wa wizara hiyo,Amon Mpanju alisema kuwa
warsha hiyo  ya siku mbili imelenga kutambua haki ya mwanamke,haki za
binadamu na haki za watoto ,walemavu na makundi mengine kuweza
kuthaminiwa .
Alisema
kuwa viongozi wa dini na Mila wanaushawishi mkubwa  katika jamii yao
,kuaminiwa hivyo hatua ya kupewa mafunzo hayo kutaisaidia serikali
katika kutokomeza vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake
na watoto vinavyozidi kushamiri miongoni mwa jamii.
“Tumieni
majukwaa yenu ya dini na  Mila kuisaidia serikali kutokomeza vitendo
vya kikatili ,unyanyasaji dhidi ya wanawake ,watoto na walemavu ,najua
mnamchango mkubwa sana kwa jamii myatumie mafunzo hayo kwenda
kuielimisha jamii kwa kukemea hadharani” Alisema
Kwa
upande wa viongozi wa dini akiwemo sheikh Hussein Junje na Mchungaji wa
kanisa la Maranatha lililopo kwa Morombo jijini hapa ,mchungaji Sadick
Kinanga walisema kuwa,watahakikisha mafunzo  hayo wanayopewa
wanayatumia  kwenda kutoa elimu   juu ya haki za sheria dhidi ya
wanawake na watoto na hatimaye kuweza kupunguza matukio ya ukatili wa
kijinsia dhidi yao.
Hata
hivyo walisema kuwa,wataweza kutumia nafasi zao kuhakikisha wanaelimisha
jamii kupinga vita matukio  hayo ya ukatili wa kijinsia kwani bado
yanaonekana kushamiri katika jamii inayotuzunguka.
Naye
Afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Arusha ,Blandina Nkini alisema
kuwa,tatizo la unyanyasaji  na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na
watoto mkoani hapa bado linaendelea kushika kasi,hivyo uwepo wa mafunzo
hayo kwa viongozi hao itasaidia sana kuibadilisha jamii kutambua umuhimu
wa  kulinda na kuheshimu haki za wanawake, watoto na walemavuy.
Mafunzo
hayo ya siku mbili yanatolewa na wizara ya sheria na katiba kwa
kushirikiana na mkoa wa Arusha ambapo yamewashirikisha viongozi hao
kutoka mikoa ya Arusha na Manyara .