Vijana watakiwa kujitoa katika taifa bila kusubiri nafasi za uongozi

Na Ahmed Mahmoud Arusha.
Vijana
nchini wametakiwa kusoma kwa bidii na kwa kufanya tafiti mbali mbali kwa
ajili ya kulisaidia taifa kufikia adhma ya uchumi wa kati wa viwanda.
Kwa
muktadha huo inabidi kujitoa kwa ajili ya kulitumikia taifa lao kwa
weledi na Uzalendo ikiwa ni pamoja na kubuni vitu mbali mbali
vitakavyolisadia taifa na kuacha Alama.
Kauli
hiyo imetolewa na Katibu wa Nec itikadi na uenezi CCM taifa Humphrey
Polepole wakati akitoa mada kwenye Darasa la itikadi kwa wanafunzi wa
vyuo na vyuo vikuu mkoani Arusha na kuwataka kujitokeza kuomba nafasi za
uongozi.
Aliwaeleza kuwa
umuhimu wa kiongozi yeyote na msomi anatakiwa kuwa mzalendo mwenye
kujituma kwa maslahi ya taifa lake bila kuwa mbinafsi na anayetazama
mchango wake kwa jamii.
“Viongozi
waadilifu wanaanzia kwenye ngazi hii mliopo ambayo kila mmoja wenu
anatakiwa kuona umuhimu wa jinsi gani ameweza kujiletea mageuzi ya
kiuchumi nchi yake kwa kutumia ubunifu alionao”alisema Polepole.
Aliwataka
kushiriki vizuri kutatua kero za wananchi bado wakiwa vyuoni kwa
kufanya tafiti bila kusubiri uongozi ambao ni mpaka nafasi ziwepo hivyo
wao wasisubiri mpaka kuambia wajitoe kwa ajili ya maendeleo ya taifa
lao.
Kwa upande wake Mnec
wa mkoa Arusha Daniel Awack aliwataka vijana hao kuwa sehe

aimu mkuu wa mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mkuu wa wilaya
ya Arumeru Jerry Muro akiongea kwenya hafla ya Darasa la itikadi kwenye
ukumbi wa hotel ya Naura Springs Jijini Hapa picha na Ahmed Mahmoud
Arusha.

 
Katibu wa CCM mkoa wa Arusha Mussa Matoroka akiogea mbele ya jumuiya ya
vijana wa vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Arusha kabla ya kumkaribisha kaimu
Mwenyekiti wa CCM mkoa na MNec Daniel Awaki kwenye Darasa la itikadi
kwenye ukumbi wa hotel ya Naura Springs Jijini Hapa.
Mjumbe wa halmshauri kuu ya CCM mkoa wa Arusha Daniel Awack akiongea
kwenye Darasa la itikadi lililofanyika kwenye ukumbi wa hotel ya Naura
Springs Jijini Arusha.picha na Ahmed Mahmoud Arusha.
Sehemu ya washiriki wa Darasa. La itikadi wakifuatilia kwa makini somo
la itikadi lililotolewa na Katibu wa Nec Taifa itikadi na uenezi
Humphrey Polepole picha na Ahmed Mahmoud Arusha
Katibu wa jumuiya ya vijana wa vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Arusha Asha
Feruzi akitoa taarifa ya Darasa la itikadi kabla ya kumkaribisha
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Baraka Mungure kwenye ukumbi wa hotel ya
Naura Springs Jijini Arusha.
Mlezi wa CCM mkoa wa Arusha na Katibu wa Nec Taifa itikadi na uenezi
Humphrey Polepole akihutubia kufungua Darasa la itikadi kwa vijana wa
vyuo na vyuo vikuu lililofanyika kwenye ukumbi wa hotel ya Naura Springs
jijini Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha.

mu ya
kukusaidia taifa letu kwa kujinga maadili na nidhamu itakawasaidia kuwa
sehemu ya viongozi watakao tukuka kwenye utumishi wao.

Alisema
kuwa msingi wa kiongozi ni uwajibikaji na kujituma kwa lengo la
kumtumikia wananchi sio kuweka ubinafsi mbele tangulizeni Uzalendo kwa
taifa lenu.
Awali Katibu
wa CCM mkoa wa Arusha Mussa Matoroka alisema kuwa jumuiya hiyo imekuwa
chachu ya mafanikio na wanajivunia kuwa na vijana wasomi ambao
watasaidia taifa na chama kuendelea kushika dola kwa kuwa na viongozi wa
wasomi.