Tcra : tunazima kidogo kwa sababu ya mambo ya kitaalamu, hauwezi ukazima laini milioni tano au 10 kwa mara moja

Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba amesema
uzimaji wa laini za simu ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole
unafanyika kwa Awamu.

Amesema zoezi hilo lililoanza jana Januari 20, 2020 linafanyika kwa
Awamu ili kuondoa usumbufu na hadi kufikia jana usiku saa nne walikuwa
wamezima laini 975,041
Amesema, kundi la kwanza waliozimiwa laini ni watu 656,091 ambao wana
Vitambulisho vya Taifa au Namba lakini hawajasajili laini zao
Amebaisha kuwa, kundi la pili ni watu 318,950 waliosajili laini zao kwa
Kitambulisho cha Taifa kabla ya kuanza mfumo wa kusajili kwa Alama za
Vidole
Amesema, “Tunazima kidogo kwa sababu ya mambo ya kitaalamu, hauwezi
ukazima laini milioni tano au 10 kwa mara moja kwa maana watajazana
kwenye kusajili kitu kinachofanya Mifumo ya NIDA inaelemewa”