Na Happiness Tesha, Mwananchi
Serikali ya Tanzania imesema itatumia
hekima kuwasaidia wananchi walioshindwa kusajili laini za simu kwa
sababu ya kukosa kitambulisho cha Taifa na namba licha ya kuanza
mchakato wa kupata kitambulisho hicho.
hekima kuwasaidia wananchi walioshindwa kusajili laini za simu kwa
sababu ya kukosa kitambulisho cha Taifa na namba licha ya kuanza
mchakato wa kupata kitambulisho hicho.
Imesema wananchi hao taarifa zao zipo katika Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa (Nida), huenda wamekosa kitambulisho au namba kwa sababu zilizo
nje ya uwezo wao.
Taifa (Nida), huenda wamekosa kitambulisho au namba kwa sababu zilizo
nje ya uwezo wao.
Hayo yameelezwa leo Jumapili Januari 19, 2020 na naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye katika mkutano wa ndani wa
CCM mkoani Kigoma.
Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye katika mkutano wa ndani wa
CCM mkoani Kigoma.
“Serikali itaona jinsi ya kutumia hekima kwa wananchi ambao taarifa zao
zipo katika ofisi za Nida kuona namna ya kufanya lakini kwa wengine
ambao hawajajaza fomu laini zao zitazimwa,” amesema Nditiye.
zipo katika ofisi za Nida kuona namna ya kufanya lakini kwa wengine
ambao hawajajaza fomu laini zao zitazimwa,” amesema Nditiye.
Amesema ambao laini zao zitazimwa ni wale waliosajili laini chache na kuacha nyingine licha ya kuwa na kitambulisho hicho.
Amebainisha kuwa usajili wa laini za simu ni endelevu licha ya baadhi ya wananchi kupuuza.
Kesho Jumatatu Januari 20, 2020 laini zote za simu ambazo hazijasajiliwa
kwa alama za vidole zitazimwa. Ili uweze kusajili laini ni lazima uwe
na kitambulisho cha Taifa au namba ya kitambulisho hicho.
kwa alama za vidole zitazimwa. Ili uweze kusajili laini ni lazima uwe
na kitambulisho cha Taifa au namba ya kitambulisho hicho.