Mataifa yaliyopoteza raia kwenye ndege ya ukraine yaidai fidia iran

Mataifa
yaliyopoteza raia katika ajali ya ndege ya Ukraine iliyodunguliwa na
Iran yameitaka Tehran iwajibike kikamilifu, uchunguzi wa kimataifa
uanzishwe na familia za wahanga zilipwe fidia.


Mawaziri
wa mambo ya nje wa Canada, Uingereza, Ukraine, Sweden, Uholanzi na
Afghanistan wamekutana jijini London katika ubolozi wa Canada.

Mawaziri
hao baada ya mkutano wao walitoa taarifa ya pamoja wakiitaka Iran
ifanye uchunguzi wa kimataifa utakao kuwa huru na wazi hasa kwa mataifa
yanayoomboleza.

Waziri
wa mambo ya nje wa Canada Francois-Philippe Champagne amesema
wamekutana  kutafuta uwajibikaji na haki kwa wahanga wa mkasa huo na
kuongeza kuwa familia za wahanga hao zinataka majibu, jamii ya kimataifa
inataka majibu na dunia nzima pia inasubiri majibu na kwamba
hawatapumzika hadi watakapoyapata.

Watu
wote 176 waliokuwa ndani ya  ndege ya abiria ya Ukraine walipoteza
maisha yao wakati ndege yao ilipodunguliwa na kombora muda mfupi baada
ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Imam Khomeini mjini
Tehran tarehe 8 mwezi huu.