Rais vladimir putin wa urusi ateua waziri mkuu mpya baada ya baraza zima la mawaziri kujizulu

Rais
Vladimir Putin wa Urusi amemteua Mikhail Mishustin kuwa waziri mkuu
mpya wa Russia. Mapema jana baraza la chini la bunge la Russia
lilipitisha uteuzi huo kupitia upigaji wa kura.


Baada
ya kuteuliwa Bw. Mishustin alitoa hotuba kwenye baraza la chini la
bunge, na kuwashukuru rais Putin na baraza hilo kwa uungaji mkono wao,
pia amesema ataripoti sera za serikali mpya kwa baraza la chini mnamo
mwezi Aprili mwaka huu.
Vilevile amewaambia waandishi wa habari kuwa atakabidhi orodha ya mawaziri kwa rais Putin hivi karibuni.

Waziri mkuu wa zamani wa Russia Dmitry Medvedev ameteuliwa kuwa naibu mwenyekiti wa Baraza la usalama la Urusi.