Kesi ya kumuondoa trump madarakani: maseneta 100 waapishwa

Maseneta 100 wa Marekani wameapishwa Alhamisi kama baraza la mahakama litakaloshughulikia kesi inayomkabili Rais Donald Trump.


Hakimu mkuu wa mahakama ya juu zaidi John Roberts aliapisha maseneta kuhakikisha wanatenda haki bila upendeleo.

Wiki
zijazo, maseneta wataamua iwapo Trump anastahili kuondolewa madarakani
kwa makosa yaliyowasilishwa na Bunge la Wawakilishi. Kesi hiyo
imepangiwa kuanza kusikilizwa Januari 21.

Hakimu
Roberts aliwauliza maseneta, ” Je mnaapa ya kwamba katika kesi
inayomkabili Donald Trump, Rais wa Marekani, ambayo inayongoja
kusikilizwa, mutatenda haki bila upendeleo kulingana na katiba, Mungu
awasaidie?”

Wabunge
wakajibu “Ndio” kabla ya kila mmoja wao kusaini kitabu walichochukulia
kiapo. Kiongozi wa waliowengi wa Republican Mitch McConnell, kisha
akaahirisha kikao cha kutathmini iwapo Donald Trump ana kesi ya kujibu
na kutangaza kwanza kesi hiyo itaanza kusikilizwa Jumanne, 13:00 EST
(18:00 GMT).

Bwana
Trump anashtumiwa kwa kutumia vibaya madaraka na kuingilia bunge. Hata
hivyo amekanusha kutekeleza makosa hayo na kusema kwamba kesi dhidi yake
ni madai dhidi yake ni ya uongo

BBC