Iran yasema mashambulizi ya leo dhidi ya marekani ni kama makofi ya uso tu

Kiongozi
mkuu wa  Iran, Ayatollah Ali Khamenei amesema hii leo kwamba shambulizi
la makombora kwenye kambi za kijeshi zinazotumiwa na Marekani nchini
Iraq ni kofi la uso kwa taifa hilo na  amesisitiza hatua hiyo ya kijeshi
haitoshi. 

Ayatollah amelihutubia taifa masaa kadhaa baada ya kushambulia kambi hizo za kijeshi.

Shambulizi
hili ni la kisasi dhidi ya mauaji ya jenerali wa kikosi maalumu cha
Quds cha Iran, Qassemi Soleimani aliyeuliwa na Marekani mjini Baghdad
Ijumaa iliyopita. 

Khamenei
amesema uwepo usio halali wa Marekani kwenye ukanda huo unatakiwa
kumalizwa akisema umesababisha vita, mgawanyiko na uharibifu. 

Waziri
wa mambo ya nje wa Iran Mohamad Zarif amesema shambulizi hilo ni sawa
na hatua za kujilinda huku rais wa halmashauri ya Ulaya Ursula von der
Leyen akitoa mwito wa kufanyika makubaliano ya kidiplomasia.