Usafirishaji wa mizigo kwa njia ya reli warejea mkoani tanga

 Meneja
wa Shirika la Reli Kanda ya Kaskazini (TRC) Ramadhani Ebrahim Gombo
akizungumza na waandishi wa habari Jijini Tanga kuhusu kurejea kwa treni
ya mizigo

 MBUNGE
wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajab akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kutembelea eneo la reli ambalo liliathirika kwa
kusombwa na maji Muheza ambalo kwa sasa limekarabatiwa na kuanza
kupitisha treni

 MBUNGE
wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajab akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kutembelea eneo la reli ambalo liliathirika kwa
kusombwa na maji Muheza ambalo kwa sasa limekarabatiwa na kuanza
kupitisha treni

 MBUNGE
wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajab katikati aliyevaa tisheti
ya mistari nyeupe akiangalia ukarabati huo ukiwa unamalizika kuendelea
eneo la Muheza ambapo kwa sasa Reli zimeanza kupita

 Mafundi wa shirika la Reli mkoa wa Tanga wakiendelea na ukarabati huo

  Greda likiendea na kazi eneo la reli Muheza kama lilivyokutwa

 Greda likiendea na kazi eneo la reli Muheza kama lilivyokutwa


HATIMAYE
usafirishaji wa mizigo kwa njia ya reli kutoka mkoa wa Tanga kwenye
mikoa ya Kanda ya Kaskazini umerejea kwenye hali yake ya kawaida baada
ya kukwama kwa kipindi cha miezi mitatu


Hatua
hiyo inatokana na daraja kubwa lililopo eneo la Muheza kusombwa na maji
mwishoni mwa mwaka jana wakati wa mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha hapa
nchini na hivyo kuleta athari kubwa.

Hayo yalisemwa jana na
Meneja wa Shirika la Reli Kanda ya Kaskazini (TRC) Ramadhani Ebrahim
Gombo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema usafiri
huo umerejea baada ya kufanyia matengenezo makubwa kwenye eneo hilo.

Alisema
kwamba baada ya daraja kubwa la reli lililopo eneo la Muheza kukatika
lilishindwa kutumika na hivyo wafanyabiashara kushindwa kuitumia kwa
ajili ya kusafirishia bidhaa zao na hivyo kusimama kwa muda.

“Daraja
la Muheza lilisombwa na Maji Octoba 10 mwaka jana na ulazimika kuanza
kunyia ukarabati kuanzia mwezi wa 11 tulianza kurekebisha kwa kuondoa
maji eneo hilo kuwawezesha wananchi kuendelea na shughuli zao”Alisema

“Lakini
baada ya hapo tulihamia maeneo mengine Korogwe,Mnyuzi, Gendagenda kwani
maeneo mengi yaliathirika na tulivyomaliza maeneo hayo 23 Novemba 2019
ndipo tuliporudi hapa muheza mpaka Januari mwaka huu tulipomaliza daraja
hilo na kwa sasa treni zinatembea na usafirishaji mizigo umerudi
kwenye hali yake ya kawaida”Alisema

Alisema kwa sasa treni
inaendelea vizuri na usafirishaji wa mizigo umerudi kwenye hali yake ya
kawaida huku akielezwa kwamba wamepata hasara kubwa kwani treni za
mizigo hazikufanya kazi ya kusafirisha mizigo na mzigo wa mingi
wanategemea kutoka Bohari ya Mafuta mkoani Tanga (GBP) na Saruji kwenda
mikoa ya Kilimanjaro, Dar na mikoa mingine Kanda ya Ziwa wamepata hasara
kubwa kwa kusombwa daraja la muheza.

Hata hivyo Mbunge wa Jimbo
la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu ambaye alitembelea eneo la reli
wilayani Muheza ambalo lililikuwa limeathirika na mvua kubwa na
kupelekea usafiri huo kusitishwa.

Alisema kwamba athari ambazo
zimetokea kutokana na kusitishwa usafiri huo ni kubwa kwa sababu daraja
hilo la reli na maeneo yote yalijaa maji na mawasiliana ya reli dar
kwenda Tanga kukatika.

Aidha alisema lakini sasa shirika la reli
wamefanya kazi nzuri sana kwa kipindi kifupi wamekuwa wakifanya kazi
kwa usiku na mchana kuhakikisha inafanya kazi.

Mbunge huyo
alisema kwamba kuanzia juzi wananchi wa Muheza wamejisikia furaha kubwa
baada ya kuanza kuona reli inapita licha ya kupatikana kwa hasara
kutokana na huduma hiyo kusitizwa kutokana na mvua kubwa zilizokuwa
zikinyesha mwaka jana na kuleta athari hiyo.

“Kama juzi juzi
mmesikia reli inapita kwenda Moshi lakini pia ilikuwa ipite na hapo
Muheza kwenda Tanga lakini kutokana na tatizo hilo imeshindwa kufika
huku lakini naamini serikali itaanzisha usafiri wa kuelekea mkoani Tanga
kwa sasa baada ya matengenezo “Alisema