Jafo ataka wanafunzi kutozuiwa kuandikishwa sababu ya kukosa vyeti vya kuzaliwa

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI

Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jafo (Mb) amesema ni marufuku mwanafunzi kuzuiliwa kuandikishwa
darasa la kwanza kwa sababu ya kukosa cheti cha kuzaliwa.

Jafo
ameyasema hayo wakati wa ziara yake Wilayani Bahi kukagua uandikishaji
wa wanafunzi wa darasa la kwanza kwa shule za msingi pamoja na mapokezi
ya wanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule za sekondari.

Jafo
amesema amepokea malalamiko kutoka baadhi ya maeneo kuwa wanafunzi wa
darasa la kwanza hawaandikishi kama hawana vyeti vya kuzaliwa.

“Nimeona
nitoe ufafanuzi kuhusu suala hili kuwa cheti cha kuzaliwa ni haki  ya
kila mtoto lakini isimzuie mtoto huyo kuanza shule eti kwa sababu tu
hajapata cheti hicho; Watoto wote wapokelewa, waandikishwe na waanze
masomo huku wazazi wao wakiendelea na mchakato wa kuwatafutia vyeti
hivyo” alisisitiza Jafo.

Sitaki
kusikia eneo lolote mtoto ameachwa kupokelewa na kuanza shule kwa
sababu ya kukosa cheti cha kuzaliwa, mzazi ahakikishe ndani ya miezi
minne amepata cheti hicho lakini mtoto huyo aanza masomo wakati masuala
ya cheti yanaendea kushughulikiwa kwenye mamlaka husika aliongeza Jafo.

Akizungumza
wakati akikagua mapokezi ya kidato cha kwanza amesema wanafunzi wote
wanatakiwa kuripoti katika muda uliopangwa na wapokelewe bila masharti
ya kuleta unga, mahindi au maharage: 

Serikali inatoa Elimmsingi bila malipo hivyo kila mwanafunzi anatakiwa kupata elimu bila bugudha ya aina yeyote.

Waziri
Jafo amepongeza uongozi wa Wilaya ya Bahi kwa umakini waliouonyesha
katika zoezi zima za uandikishaji wa darasa la kwanza linaloendelea na
maandalizi mazuri katika mapokezi ya kidato cha kwanza, halkadhalika
katika usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya
hiyo.

Akizungumza
wakati wa ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Mwanahamisi Munkunda
amesema katika Halmashauri ya Bahi walishafanya kampeni ya upatikanaji
wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano
hivyo watoto wengi wanaonza shule hivi sasa wanavyo vyeti hivyo na
endapo mtoto yeyote atakua hajapa basi ataandikishwa shule ndipo
mchakato kwa cheti utafuata.

Kwa
upande wa mapokezi ya kidato cha kwanza amesema wanafunzi
waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika Wilaya ya Bahi ni
2712 na changamoto iliyopo ni uhaba wa madawati ambayo wameshaanza
kuitatua kwa kuchonga madawati yatakayokidhi idadi ya wanafunzi hao

Naye
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mkakatika John Laurent Josephat amesema
shule yake ina malengo ya kaundikisha wanafunzi 180 na kwa siku ya
kwanza tu shule ilivyofunguliwa wameandikisha wanafunzi 134.

“Wanafuzi
wote walioletwa shuleni kwetu tumewaandikisha na endapo mtoto hana
cheti cha kuzaliwa tulitumia kadi la Kliniki kupata taarifa sahihi za
mtoto na hatujarudisha mwanafunzi hata mmoja wote wamewpokelewa na
wameanza masomo” Alisema Mwl. Josephat.

Aliongeza
kuwa uandikishaji huu kwa siku ya kwanza tu ni zaidi ya aslimia 70
hivyo anategemea tutaandikisha zaidi ya malengo waliyojiwekea.

Shule
ya msingi Mkakatika ni miongoni mwa shule bora katika Wilaya ya bahi na
ndiyo iliyoongoza kwa kuwa shule ya kwanza kiwilaya katika matokeo ya
darasa la saba kwa mwaka 2019