Trump atishia kuiwekea iraq vikwazo kama itawafukuza wanajeshi wa marekani

Rais
wa Marekani, Donald Trump, ametishia kuiwekea Iraq vikwazo baada ya
bunge la nchi hiyo kupiga kura kupitisha azimio linalovitaka vikosi vya
Marekani viondoke nchini humo. 


Trump amesema iwapo wanajeshi hao wataondoka, Iraq itapaswa kuilipa Marekani gharama za kambi ya jeshi la anga iliyoko Iraq. 

Trump
amebainisha kuwa hawatoondoka hadi hapo Iraq itakapoilipa Marekani
gharama za kambi hiyo ambayo amesema iko muda mrefu hata kabla ya wakati
wake na iligharimu mabilioni ya dola kuijenga.

 Trump
amesema kama Iraq itavitaka vikosi vya Marekani kuondoka na suala hilo
kufanyika katika njia isiyokuwa na misingi ya kirafiki, basi nchi yake
itaweka vikwazo vikali kwa Iraq ambavyo haijawahi kushuhudia.

 Wakati
huo huo, Ikulu ya Marekani imesema kuwa Trump amezungumza na Waziri
Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson kuhusu hali inayoendelea nchini Iraq na
Iran.


Soma hii: Ajira Mpya 250+ zilizotangazwa wiki hii


Mvutano
bado ni mkubwa baada ya Marekani kuusika kumuua kiongozi wa jeshi wa
Marekani jenerali Qasem Soleimani huko Baghdad wiki iliyopita.

Soleimani ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 62, alikuwa akiongoza operesheni za vita katika nchi za mashariki ya kati


Kiongozi mpya wa kikosi cha jeshi la Iran la Quds – ambacho Soleimani
aliongoza – ameapa kuwaondoa Wamarekani katika mataifa ya mashariki ya
kati.