Jeshi la kenya lazima shambulizi la al-shabaab lamu…wanne wauawa

Jeshi
la Ulinzi la Kenya (KDF) limetangaza habari ya kuwaua  wanachama wanne
wa kundi la kigaidi la al-Shabaab katika kaunti ya Lamu, kusini
mashariki mwa Kenya, mpakani na Somalia.


KDF
imesema katika taarifa kuwa, hakuna askari au raia aliyeuawa katika
shambulizi hilo lililofeli la alfajiri ya leo mwendo wa saa kumi na
moja, dhidi ya kambi ya jeshi iliyoviziwa na wanamgambo wa al-Shabaab,
karibu na uwanja mdogo wa ndege wa Manda, eneo la Magogoni.

Kamishna
wa Kaunti ya Lamu, Irungu Macharia amethibitisha kutokea uvamizi huo
ambao al-Shabaab imekiri kuhusika nao. Hata hivyo Jeshi la Ulinzi la
Kenya limefanikiwa kuzima shambulizi hilo kwa kutumia ndege ya kijeshi.

Duru za habari zinaarifu kuwa, kambi hiyo ya kijeshi ina askari wa Kenya na Marekani.

Haya
yanajiri siku chache baada ya wapiganaji wa kundi hilo la kigaidi
kuteka nyara basi la abiria katika kaunti hiyo ya Lamu, na kuua watatu
miongoni mwao.

Siku
ya Ijumaa, wanamgambo wasiopungua 33 wa kundi la kigaidi la al-Shabaab
waliangamizwa katika operesheni mbili tofauti za jeshi kusini magharibi
mwa Somalia.