Waziri kigwangalla : kuleta kiburi na jeuri kwenye mazingira haya ni upumbavu

Baada
ya Rais John Magufuli kuagiza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.
Hamisi Kigwangalla pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Adolf
Mkenda kumaliza tofauti zao vinginevyo atawaondoa, Kigwangalla ameibuka
na kudai kuwa tayari walishamaliza tofauti zao na sasa hali ni shwari.

Kupitia akaunti yake ya Twitter na Instagram  amesema walishafanya kikao
na Katibu Mkuu, Prof. Adolf Mkenda cha kumaliza tofauti zao.

“Kazi ya Urais ni ngumu sana, tulioteuliwa na Rais kumsaidia
utendaji/usimamizi wa maeneo mbalimbali hatupaswi kumuongezea
frustrations nyingine zaidi, sisi kwenye Wizara yetu, baada ya kikao na
Chief Secretary tulimaliza tofauti zilizokuwepo na sasa hali ni shwari,”
amesema Kigwangalla.
Ni imani na heshima kubwa sana kwako kuteuliwa kuwa Waziri kwenye
nchi yako. Kwenye nchi ya watu milioni 60, kwa nini Hamisi KIGWANGALLA?
Sijui. Ni neema na baraka za Mungu tu. Maana siyo kila mtu kwenye maisha
yake atapata fursa ya kuhudumu kwenye serikali kama Waziri ama kama
Katibu Mkuu kwenye serikali. Siibezi wala siwezi kuichezea fursa hii
adhimu.
Ni kwa kuelewa ukweli huu na ushauri, mwongozo na maelekezo ya wakuu
wa kazi, na watendaji wazoefu kwenye utumishi wa umma, kama Katibu Mkuu
Kiongozi, tulikaa mimi na Katibu Mkuu wangu na kukubaliana kufungua
ukurasa mpya wa mahusiano mazuri zaidi kwa manufaa ya nchi yetu.
Kuondolewa kwenye nafasi ya Uwaziri unaweza kuondolewa kwa sababu
mbalimbali lakini kuondolewa kwa sababu watu wazima, tena viongozi,
ambao mmepewa fursa ya kushauriwa, mmeshindwa kuelewana, ni upumbavu!
Mimi siyo mpumbavu.
Kuleta kiburi na jeuri kwenye mazingira Haya ni upumbavu. Kwanza sisi
waislam tunafundishwa kuwa wanyenyekevu, maana ‘kiburi’ ni sifa ya
Mungu, siyo yetu wanadamu. Kufanya kiburi na jeuri ni upumbavu. Hekima
ya Mungu ni kujishusha na kumshinda shetani.
Sina jeuri wala kiburi sababu nimelelewa vizuri na bibi yangu Mama
Bagaile, na pia naogopa hasira za Mungu. Tumalizie haya masaa kwa amani!
Happy New Year Good People. Nitaendelea kutoa darasa la mambo
niliyojifunza 2019, na mipango yangu ya 2020.
Nipo jimboni nachunga ng’ombe wangu kidogo. Ningekuwa Dar
ningemtembelea Prof. Mkenda kwa ajili ya picha tukigonga glass ili mjue
tuko sawa 😀. Mhe. Rais yeye ana namna yake ya kupata taarifa zetu.
Atazipata tu! 😀. Limeisha hilo au niongeze volume? 🤷🏾‍♂️ Wakatabahu
Dkt. Hamisi KIGWANGALLA, MB., MNEC, WMU.