Katibu mkuu chadema, mheshimiwa john mnyika leo amesimikwa kuwa chifu wa wasukuma na kupewa jina la maronja likiwa na maana ya mrekebishaji. mnyika yupo mapumzikoni kijijini kwao mkoani mwanza.

Rais
Magufuli amewasilisha fomu ya tamko kuhusu Rasirimali na Madeni katika
ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyopo Dar es
Salaam.

Fomu
hizo zimewasilisha leo Jumapili Desemba 29, 2019 na katibu wake, Ngusa
Samike kwa niaba ya Rais Magufuli aliyepo wilayani Chato mkoani Geita
kwa mapumziko.

Akipokea
fomu hizo, Kamishna wa Maadili, Jaji mstaafu Harold Nsekela amempongeza
Rais Magufuli kwa hatua hiyo akisema ametekeleza matakwa ya Kikatiba na
Sheria ya Maadili.

“Viongozi
kurejesha tamko ni jambo la kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 132 (5)b.
Ibara hii inasema msingi wa maadili wa viongozi wa umma, itawataka watu
fulani walioshika nafasi fulani za madaraka kutoa mara kwa mara maelezo
kuhusu mapato, rasirimali na madeni yao.

“Katiba
ndiyo inatatuka sisi viongozi kutoa maelezo haya kila mwaka. Ukija
katika sheria yetu namba 13 ya mwaka 1995 kifungu 9 inaeleza kila mwisho
wa mwaka kiongozi anatakiwa kumpelekea kamishna tamko la maandishi,”
amesema Jaji Nsekela.

Jaji
Nsekela amempongeza Rais Magufuli kwa kurejesha tamko la mapato, madeni
na rasirimali zake kama kiongozi wa umma, huku akiwataka viongozi
wasiorejesha kufanya hima kutekeleza mchakato huo kwa sababu zimebaki
siku mbili pekee.