Shilingi bilioni 1.8 za chenchi ya vifaatiba, dawa,na vitendea kazi kutumika kwa maendeleo na kuboresha huduma bmc

Askari wa Usalama
barabarani akiwaongoza maandamano ya watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya
Kanda , Bugando pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu Katoliki cha Sayansi
za Tiba na  Afya (CUHAS)  wakiadhimisha Siku ya Bugando Day jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali
ya BMC ya jijini Mwanza, Profesa Abel Makubi, kulia akifungua moja ya
makufuli yaliyofungwa kwenye moja ya  kontena la vifaa tiba ,dawa na
vitendea kazi kati ya makontena sita, baada ya kuwasili nchini na
kupokewa jana na uongozi wa hospitali hiyo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
Katoliki  cha Sayansi za Tiba za Afya (CUHAS) Profesa Paschalis
Rugarabamu (kushoto) akikata utepe kuashirikia kupokea makotena ya vifaa
tiba, dawa na vitendea kazi vya Hospitali ya Rufaa ya Kanda,  Bugando
(BMC) vilivyonunuliwa kwa sh. bilioni 1.2 baada ya kuwasili nchini
kutoka China.Kulia ni Mkurugenzi wa   hosptali hiyo Profesa Abel Makubi.
Mkurugenzi
wa Huduma za Upasuaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda , Bugando (BMC)
Dk. Fabian Massaga (mwenye kofia wa tatu kutoka kushoto) akitoa
ufafanuzi wa kotena moja kati ya sita ya vifaa tiba na madawa baada ya
kuwasili na kupokelewa na Vvongozi na watumsihi wa hospitali hiyo jana, 
na watumishi.
Wa tatu kutoka kulia mwenye suti ya michezo ni Mkurugenzi wa hospitali hiyo Profesa Abel Makubi.
****************************
 NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
HOSPITALI
ya Rufaa ya Kanda,Bugando Medical Centre (BMC) imesema fedha zaidi ya
sh. bilioni 1 zilizobaki kwenye manunuzi ya vifaa tiba,madawa  na
vitendeakazi zitatumika kwa shughuli za maendeleo na kuboresha huduma
mbalimbali za hospitali.
Mkurugenzi
Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Abel Makubi alisema jana wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Bugando (Bugando Day) muda mfupi baada ya kupokea
moja ya makontena kati ya sita ya vifaa hivyo vilivyogharimush. bilioni
1.2 kati y ash. bilioni 3 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili hiyo.
Alisema
hospitali  ya BMC ilikuwa na changamoto ya vifaa tiba na dawa na hivyo
kuzua malalamiko kutoka kwa wagonjwa jambo lililousukuma uongozi na
menejimenti kutafuta suluhu ya changamoto hiyo ambapo walishindanisha
kampuni mbalimbali ili kujua bei ya vifaa tiba na madawa
kulingana  mahitaji kabla ya kuagiza.
 “Ili
kupunguza chagamoto hiyo uongozi na menejimenti ya
hospitali  tulikubaliana kutumia fedha za ndani kuagiza vifaa tiba,
madawa, vitendea kazi na sare za watumishi kwa gharama ya sh. bilioni
1.2  kutoka nchini China na kuokoa kiasi kikubwa cha fedha, endapo
tungenunua hapa nyumbani ingetugharimu sh. bilioni 3,”alisema Profesa
Makubi.
Alisema  kununua
madawa na vifaa tiba nje kwa gharama nafuu wameokoa fedha nyingi
wanazokusanya na kutumia kidogo lengo likiwa ni kuboresha huduma za tiba
kwa wananchi na vitasaidia pia changomoto ya hospitali nyingi za umma
kwa sababu zina matatizo ya vifaa tiba.
Alishauri
taasisi za umma kulinda na kutumia kidogo wanachopata ili wananchi
wapate huduma bora kwa kununua vitendea kazi katika kuboresha huduma  na
kuzifanya kuwa bora.
“Ili
kukabiliana na changamoto ya vifaa ni kuboresha huduma wananchi watibiwe
kwa vifaa bora na katika mazingira bora, si vifaa tu hata mahali
wagonjwa wapolala, hilo ndilo BMC tumefanya,”alisema Profesa Makubi.
Mkurugenzi
huyo wa BMC alisema baada ya kupata vifaa tiba vya kisasa vya vipimo na
upasuaji wa kibingwa kutaharakisha utoaji wa huduma na kwa ufanisi
zaidi, kutaokoa muda na majibu kupatikana haraka badala ya mgonjwa
kusubiri kwa saa mbili.
Dk.
Makubi alitaja miongoni mwa vifaa tiba walivyopata kuwa ni mashine 6 za
Utra Sound na vifaa vya upasuaji ambavyo vitawezesha wagonjwa
kuchunguzwa na kufanyiwa upasuaji kwa haraka zaidi na kupunguza
malalamiko ya kuchelewa kuhudumiwa.
Aliwataka
watumishi wa hospitali hiyo wakiwemo wanaohudumu kwenye hospitali za
serikali kujituma zaidi kuwahudumia wananchi haraka na kwa ubora kwani
hiyo ndiyo rai ya menejimenti ya BMC na watumie lugha safi kwa wagonjwa.
“BMC
tunawathamani watumishi kwa kuwapa faraja waone utendaji wao
unathaminiwa, hii itawatia moyo na hamasa, hivyo kuwafanya wajitume
zaidi kwa wananchi na kuhakikisha wanapata huduma bora za
kiwango,”alisema Profesa Makubi.
Awali
Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dk.  Fabian Massaga, alisema shilingi
bilioni 1.8 kati ya bilioni 3 zilizookolewa kwenye ununuzi wa vifaa
tiba na madawa zitatumika kwa maendeleo na kuboresha huduma mbalimbali
za hospitali.
Alivitaja
baadhi ya vifaa tiba ni vitanda, mashine sita za Utra Sound,vifaa vya
upasuaji (operating set), madawa mbalimbali, kompyuta zitakazounganishwa
na mfumo na kuondokana na madaktari kutumia majadala kwa ajili ya
kumbukumbu za wagonjwa na sare za watumishi vyote vikigharimu sh.
bilioni 1.2 fedha za ndani.
Aidha,
katika hatua nyingine Profesa Makubi, alisema wanapoadhimisha  Siku ya
Bugando Day mwaka huu lengo ni kuwakumbusha watumishi wa  Hospitali ya
BMC  majukumu yao, kuonyesha umoja na mshikamano kati yao na watumishi
wa Chuo Kikuu Katoliki cha Sayansi za Tiba za Afya (CUHAS).   
Kwa
upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha CUHAS, Profesa Paschalis
Rugarabamu,alisema wanashirikiana chuo na hospitali kujenga maadili na
kuhimiza vijana kutimiza majukumu yao ya utoaji wa huduma za tiba kwa
kuzingatia maadili ya kitaaluma ingawa ni kazi ngumu.
Pia
wamepanua wigo wa taaluma nje ya BMC kwa kuwapeleka wanafunzi wa chuo
hicho kujifunza kwenye maeneo tofauti licha ya matakwa ya mtaala
wanafanya mazoezi katika mazingira halisi kwa kuzijengea uwezo wa elimu
na huduma katika hospitali za Sekou Toure na Sengerema DDH.
Hospitali
ya Bugando iliyojengwa mwaka 1967 kwa msaada wa Serikali ya Ujerumani
Magharibi kwa ushirikiano na Uholanzi kupitia shirika moja la kikatoliki
ambapo mwaka huu imeadhimisha miaka 52 na  ilifunguliwa, Desemb 3, 1971
na Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius K. Nyerere