Serikali yatoa siku 60 kampuni ya songoro ikamilishe kuunda boti ya mafunzo

Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditie akizindua boti ya Ukoaji iliyopo
nyuma yake,Pmbeni yake upande wa Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha baharia
Daktari Erick Massami na Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya Chuo hicho
Captain Ernest Bulamba.
Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditie akitoa hotuba
wakati wa mahafali ya 15 ya Chuo cha baharia (DMI) jijini Dar es Salaam
Wahitimu wa Chuo cha bahari wakisubiri kutunukiwa vyeti vyao.


Na Hellen Isdory Dar es Salaam

Serikali imetoa siku 60 kwa Kampuni ya Kuunda Meli ya Songoro
kukamilisha boti ya mafunzo kwa vitendo ambayo ina uwezo wa kubeba watu
180 ili ianze kazi haraka.
Akizungumza leo Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi
Atashasta Nditie kwenye uzinduzi wa boti ya Uokoaji sambamba na
mahafali ya 15 ya Chuo cha baharia (DMI) jijini Dar es Salaam alisema
Mkandarasi huyo pesa alishapewa yote na serikali lakini hadi sasa
hawajamaliza.
Mhandisi Nditie alibainisha kuwa boti hiyo ni muhimu kwa wanafunzi
wanaosomea uhandisi na ubaharia hasa katika kusoma kwa Vitendo hivyo
kuto kuwepo kwa wakati kunasababisha masomo yao yasifikie kiwango kizuri
cha ufaulu.
“Ninazo taarifa kuwa chuo hiki kimepewa meli nzuri na mdau wa Maendeleo
na nyie mmempa mkandarasi aitwaye Sorongo lakini hadi sasa
hajakamilisha na inasemekana ni miezi miwili hajafika eneo la kazi
naomba mumpe taarifa nataka hiyo meli ndani ya miezi miwili kuanzia
sasa”,alisema.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi chuoni hapo Dkt.
Ernest Bupamba alibainisha kuwa chuo hicho ni kikubwa na kinatoa
mafunzo ya ubaharia kwa kiwango cha kimataifa na hadi sasa kimethibitika
kimataifa katika viwango vya ubora.
“Chuo hiki ni kikubwa kwa Ukanda mzima wa Afrika na kimeweza kuwa kituo
cha ubora katika ukanda wa Afrika mashariki na kusini mwa jangwa la
sahara”,alisema.
Chuo hicho hadi sasa kinauwezo wa kubeba wanafunzi 693