Picha: rais magufuli alivyopokelewa kwa shangwe uwanja wa ccm kirumba

Rais
Magufuli ameingia Uwanjani wa CCM Kirumba Mwanza jijini Mwanza huku
akipokewa kwa shangwe na vigeregere kutoka kila kona ya uwanja huo
uliofurika.



Rais
Magufuli aliingia uwanjani hapo saa 3: 14 asubuhi leo Jumatatu Desemba
9, 2019 akiwa kwenye gari la wazi akiongozwa na pikipiki nane gari moja
mbele na nyingine nyuma.


Ameingilia
mkono wa kushoto mwa uwanja na kuuzunguka akiwapungia wananchi mikono
huku akishangiliwa kila alipopita wakati ukiimbwa wimbo wa taifa.