Rais magufuli na viongozi wengine wa kisiasa waomboleza kifo cha ali mufuruki

 Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli  amepokea kwa
masikitiko makubwa taarifa za  kifo cha Mfanyabiashara maarufu hapa
nchini, Ali Mufuruki, aliyefariki Dunia akiwa nchini Afrika ya Kusini.



Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Kijamii wa Twitter, leo Desemba 8, 2019, ameandika;  Nimehuzunishwa
na taarifa za kifo cha rafiki yangu Ali Mufuruki (Mwenyekiti na
Mwanzilishi wa Jukwaa la Wakurugenzi Watendaji wa Kampuni – CEOrt)
Nitamkumbuka kwa uzalendo na mchango wake katika kukuza sekta ya
biashara na ushauri kwa Serikali.Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un.


Mbunge
wa Kigoma Mjini, na kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe
ameandika; “Sina maneno ya kusema zaidi ya kuwa sote ni wake Mwenyezi
Mungu na kwake sote tutarejea, sio tu alikuwa rafiki bali alikuwa
mshauri wangu, tulipishana mawazo fulani lakini alikuwa na heshima
kubwa, tangulia ndugu yangu RIPMufuruki” 


Mwanasiasa
mwingine aliyeonesha kuguswa na msiba wa Ali Mufuruki ni mwanasiasa wa
muda mrefu Khamis Kagasheki, ambaye ameandika hivi; “Kwa mshtuko na
masikitiko nimepata taarifa kwa kifo cha Ndg Ali Mufuruki, pigo kubwa
kuondokewa na Ali, mkono wa pole nyingi kwa familia yake, MwenyeziMungu
amhurumie na amsamehe. Ali you will be missed immensely”.


Nape
Nnauye yeye kaandika; Ni kazi ngumu sana kusimamia kile unachoamini
hasa kama kitendo hicho kitakufanya msielewane na marafiki na watu wako
wa karibu, LAKINI wewe Ally Mfuruki uliweza kuwa imara na mkweli kwa
ulichoamini! Pumzika kwa amani!”

Kwa
upande wake Maalim Seif yeye kaandika; “Nimepokea kwa huzuni,
masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Ndugu Ali Mufuruki @amufuruki
kilichotokea jana katika Hospitali ya Morningside, Johannesburg, nchini
Afrika Kusini. Mwenyezi Mungu Amlaze mahala pema Peponi. Amin. Hakika
sisi ni wa Mungu na Kwake Yeye Tutarejea.”


Wengine walioguswa na kutuma salamu za pole kwa ndugu jamaa na marafiki
wa mfanyabiashara huyo ni pamoja na Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini
Tanzania.
Ali Mfuruki aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Vodacom
Tanzania, aliyehudumu kwa muda wa miaka miwili, ambapo baadaye
alitangaza kujiuzulu nyadhifa zake zote