Tcra kampeni ya mnada kwa mnada wilayani babati katika utoaji wa elimu ya usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole

Wananchi wakihudumiwa usajili wa Laini za simu wakati Kampeni ya Mnada
kwa Mnada wa TCRA uliofanyika Viwanja vya Magugu wilayani Babati mkoani
Manyara
Wananchi wakipata huduma ya usajili wa Laini za simu wakati Kampeni ya
Mnada kwa Mnada iliyofanyika Viwanja vya Magugu wilayani Babati mkoani
Manyara
Mwananchi akisajili laini ya simu kwa alama za vidole moja ya Kampuni ya
huduma za Simu za Mkononi wakati wa Kampeni ya Mnada kwa Mnada
uliofanyika Viwanja vya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara.
Mkuu wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Mhandisi Emelda Salum akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Babati mkoani
Manyara wa Katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada iliyofanyika katika
Viwanja vya Stendi ya Zamani ya mabasi ya Magugu ya usajili wa Laini za
Simu kwa Alama za vidole
Afisa Habari Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akitoa maelezo kwa Wananchi wa Babati.
Wakazi wa wilayani Babati  mkoani Manyara  na viunga
vyake  wamejitokeza katika kupata namba za vitambulisho vya Taifa ili
kukidhi matakwa ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania TCRA ipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya
 Uhamasishaji wa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole na
kuongeza kuwa ambaye hatatimiza matakwa ya kisheria ya kusajili laini ya
simu kwa alama za vidole laini hiyo  itafungwa


Kampeni
 ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu
Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya
Uhamiaji  kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa
kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa
kuweka alama za vidole kwa laini za simu.
Kampeni
tangu imeanzishwa imekwenda katika maeneo ya miji na Mkoa lengo Wananchi
kutumia fursa ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole ambayo
unakwenda nchi nzima 

Akizungumza
na Wananchi wa Wilaya ya Babati katika Stendi ya mabasi ya Zamani ya
Magugu Mkuu wa Kanda ya Kasikazini wa  TCRA  Mhandisi Emelda Salum
amesema ni fursa kwa wananchi wa Babati  na maeneo Mbalimbali wamefika
katika Viwanja vya Stendi ya Zamani ya Magugu kupata namba ya
kitambulisho cha Taifa katika mfumo wa NIDA na kuweza kusajili laini ya
simu kwa alama za vidole.

 Mhandisi
Salum Amesema katika Kampeni hiyo imekuwa inafanywa na kanda hiyo ikiwa
 kila mwananchi aweze kuwa na namba ya Kitambulisho au Kitambulisho cha
 Taifa  kutokana Ushirikiano na NIDA kuwa katika Kampeni hiyo.
  
Amesema
kuwa  Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi
kuhudumiwa kwa pamoja  kwa huduma za mawasiliano na usajili wa laini za
simu kwa alama za vidole.

Amesema
Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika  huduma  za simu pamoja
kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi na kuongeza kuwa muda
ulioabakia ni 27 mdogo hivyo kila mtu atumie kutafuta taarifa
zinazokidhi usajili wa laini kwa alama za vidole.


Hata
hivyo amesema  kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa
elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto
wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Hata hivyo amesema kuwa
 kuna
watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi
Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kutoa elimu kuhusiana
 makosa ya jinai ya matumizi ya simu yasiofuata sheria.

 Kampeni
hiyo ni endelevu katika kuwafikia wananchi kuhakikisha kila mwananchi
anasajili laini  ya simu kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho
cha taifa au namba ya kitambulisho hicho.

Salum
 amesema kuwa  TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili
watumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa kupitia
Kampeni ya Mnada kwa mnada.

Hata
hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze  kujisajili kwa alama za vidole
kabla ya Desemba 31 kwa kufika katika maduka  ya watoa huduma wa Kampuni
za Simu za Mkononi.

“TCRA
tutahakikisha tunawafikia  wananchi wote kupata  elimu ya  utumiaji wa
bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo” amesema
Mhandisi Salum.

Ameongeza kuwa  Kampeni iko katika mikoa yote iliopo katika kanda ya Kaskazini.

Nae
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA  Makao Makuu Mabel Masasi amesema
kuwa wananchi wameitikia kwa kujitokeza kwa wingi  kuangalia namba
 vitambulisho kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole na
wengi wamepata namba hizo  na kufanya usajili kwa watoa huduma wa
Kampuni za Simu za Mkononi.

Masasi
amesema kuwa Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA
kupata elimu na baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende katika
mamlaka husika kupata utaratibu wa  vitambulisho vya Taifa.