WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemtaka mkandarasi anayejenga machinjio ya kisasa
ya Vingunguti jijini Dar es Salaam ahakikishe kwamba anakamilisha
ujenzi huo mwishoni mwa mwezi huu kama alivyoamriwa na Rais Dkt. John
Pombe Magufuli.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo leo (Jumanne, Desemba 3,
2019), Mheshimiwa Majaliwa amesema amefurahishwa na hatua ya mkandarasi
huyo ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ya kuongeza idadi ya
watalaam na mafundi ili kuhakikisha kwamba kazi hiyo inafanyika haraka
na kukamilika kwa wakati ulioamriwa na Rais Magufuli yaani Desemba 30,
mwaka huu.

Amesema amefurahi pia kuona kwamba mkandarasi huyo ameamua kufanya kazi
usiku na mchana, hatua ambayo imeongeza kasi ya ujenzi huo na anaamini
kuwa kazi hiyo itakamilika kwa wakati.

Mheshimiwa Majaliwa amemtaka Mshauri Mwelekezi wa mradi huo ambaye ni
M/SCONS AFRIKA LIMITED na FB Consultant wa Dar es Salaam asimamamie kwa
karibu ili kujiridhisha kuwa maelekezo yote yaliyopo kwenye michoro
ya ujenzi huo yanazingatiwa na mkandarasi.

Amesema Serikali imeamua kujenga machinjio hayo ya kisasa ya Vingunguti
baada ya kugundua kwamba wafanyabiashara wa mifugo na mazao yake katika
machinjio hayo, walikuwa wakifanya kazi zao kwenye mazingira duni na
kwamba nyama iliyokuwa ikitoka kwenye machinjio hayo ilikuwa haikubaliki
kwenye soko la nje ya nchi.

“Uamuazi wa Serikali kujenga machinjio haya, utaifanya nyama inayotoka
hapa ikubalike kwenye masoko ya nje ya nchi, hatua ambayo itaongeza
mzunguko wa fedha kwenye eneo hili wakati Serikali na Manispaa
watanufaika kwani kutakuwa na ongezeko la makusanyo ya kodi,” aliongeza
Mheshimiwa Majaliwa.

Waziri Mkuu pia ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na
Manispaa ya Ilala wafanye mazungumzo na uongozi wa Shirika la Reli
Tanzania (TRC) ili ijengwe reli ya mchepuko kutoka reli ya kati kwenda
kwenye machinjio ya Vingunguti ili mifugo iingizwe moja kwa moja kwenye
machinjio hayo badala ya kuteremshiwa Pugu halafu ikapelekwa kwa
magari.

Amewahakikishia wafanyabiashara wote wanaoendesha shughuli zao kwenye
machinjio hayo kuwa ujenzi wa machinjio ya kisasa ya Vingunguti
hautawafanya wapoteze fusa zao za biashara au kuajiriwa kwenye eneo hilo
kwani machinjio hayo yatafungua fursa zaidi za biashara na ajira kwao.

Amewaagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala
wahakikishe kwamba wanaushirikisha uongozi wa wafanyabiashara wa mifugo
na mazao yake wa Vingunguti ili wanachama wao wenye sifa za kuajiriwa,
waajiriwe na pia wawaandalie mazingira ya kufanya biashara mbalimbali
karibu na machinjio hayo.

Akizungumzia soko na bei duni ya ngozi za mifugo nchini, Waziri Mkuu
amekemea tabia ya wafugaji ya kuweka alama kwenye ngozi za mifugo yao
hasa ng’ombe kwani kufanya hivyo kunashusha thamani ya ngozi za Tanzania
na badala yake amewataka waweke alama za hereni kwenye masikio ya
mifugo yao ili kulinda ubora wa ngozi za mifugo yao.

Amesema Serikali tayari imekwishampata mwekezaji kutoka Misri ambaye
amekubali kuwekeza kwenye kiwanda cha ngozi cha Mwanza hatua ambayo
italihakikishia Taifa soko la ngozi.

Mapema, akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,
Jumanne Shauri amesema ujenzi wa machinjio hayo ulianza Julai 8, mwaka
huu na mkandarasi alitakiwa akamilishe ujenzi huo ifikapo Januari 6,
2021. Amesema kufuatia agizo la Rais Magufuli alilolitoa Septemba 16,
mwaka huu, ujenzi huo unatakiwa ukamilike ndani ya miezi mitatu yaani
ifikapo Desemba 31, 2019.

Bw. Shauri amesema awamu ya kwanza ya ujenzi wa mradi huo itagharimu
sh. 12, 498,916,063.00 ambapo sh. 8,528,486,470.00 ni ruzuku kutoka
Serikali Kuu na sh. 3, 970,429,593.00 zimetokana na mapato ya ndani ya
Halmashauri na kwamba ujenzi wa mradi huo kwa sasa umefikia asilimia 60.

Akisoma risala ya Ushirika wa Wafanyabiashara ya Mifugo na Mazao yake
wa Vingunguti (UWAMIVI), Mwenyekiti wao, Bw. Joel Meshaki aliiomba
Serikali iwaandalie wafanyabiashara hao eneo mbadala la kufanyia
shughuli zao ili ajira yao isipotee.

Alipendekeza kwa Waziri Mkuu maeneo matatu yaliyoko karibu eneo hilo,
ambayo yangewafaa wafanyabiashara hao wakati watakapoondoka kwenye
maeneo yao sasa yanapojengwa machinjio ya kisasa kuwa ni Dampo la zamani
ambalo kwa sasa halitumiki, eneo la Wizara ya Kilimo ambalo kwa sasa
ni sehemu ndogo tu inayotumika na jengo la Kilimo ambalo kwa sasa
linatumika kama ghala.

Alisema idadi ya mifugo inayochinjwa katika machinjio hayo kwa sasa ni
ng’ombe 550 hadi 600 kwa siku za kawaida na siku za sikukuu ni ng’ombe
1,000 hadi 1,500. “Halmashauri yetu ya Ilala hukusanya zaidi ya sh.
milioni 118 kwa mwezi wakati Serikali Kuu hukusanya milioni 117 kila
mwezi,” alisema Meshaki.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU