Elimu ya umeme kwa wasioona yaipa tanesco taswira mpya

 MKUU wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare  akizungumza wakati wa uzinduzi wa wasrha hiyo kushoto ni  Kaimu meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro William Masome

 Sehemu ya wanachama wa chama cha wasioona  Tanzania (TLB)  mkoani Morogoro.

 Sehemu ya wanachama wa chama cha wasioona  Tanzania (TLB)  mkoani Morogoro Mkuu wa Mkoa huo ambaye hayupo pichani

 wanachama wa chama cha wasioona  Tanzania (TLB)  mkoani Morogoro.

MKUU wa Mkoa wa Morogoro aliyevaa suti jeusi akiwa kwenye picha ya Pamoja na washiriki wa semina hiyo kushoto ni  Kaimu meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro William Masome 

SHIRIKA
la Umeme Nchini TANESCO limeendesha semina maalum inayohusu masuala ya
Umeme kwa wanachama wa chama cha wasioona  Tanzania (TLB)  mkoani
Morogoro.

Akizungumza
wakati wa uzinduzi  wa warsha hiyo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  Loata Ole
Sanare amesema kuwa Tanesco  imeonyesha mfano mzuri wa kuigwa kwa kutoa
elimu hiyo kwa watu wa kundi  maalum katika jamii.

Alisema
pia kupitia hili shirika limetoa taswira kuwa mashirika ya Umma
yanafuata muelekeo wa Raisi John Pombe Magufuli ambae ni  Raisi wa
wanyonge na kwa kujali wateja wake hata wa Makundi maalum kwa kutoa
elimuYa Umeme itakayowasaidia katika maisha yao ya kila  siku.

Mkuu
huyo wa Mkoa  amewataka wasioona kutokuwa wanyonge kwakudhani kuwa 
Serikali haiwatambui na kusema kuwa Serikali ipo pamoja nao na
kuwakaribisha katika ofisi za Mkoa, muda wowote watakapokua na
changamoto zozote.
Naye
Kaimu meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro
William Masome amesema Kuwa TANESCO chini ya Mkurugenzi Mtendaji Dkt.
Tito Mwinuka imetambua umuhimu wa watu wenye Ulemavu wa kutoona kupatiwa
elimu ya Umeme ili waweze kutambua fursa  zitokanazo na umeme
zitakazoweza kuwainua kiuchumi lakin pia kuwafundisha jinsi ya kutumia
umeme vizuri (matumizi Bora ya umeme)ili wasilipe gharama kubwa
Kwenye kununua Umeme.

Naye
kwa upande wake Mratibu wa idara ya maendeleo, Vijana na Chipkizi toka
TLB , Bw.Kiongo Itambu ameishukuru TANESCO kwa kuwapatia elimu hiyo
Maalum ambayo itawasaidia hasa katika kujiepusha na matukio ambayo yanaweza kuathiri usalama wao.

Alisema
kwani wameshajua athari za kukaa karibu na miundombinu ya umeme  na 
kuahidi kushirikiana na TANESCO katika kuwafichua wanaolihujumu Shirika
kwa kuiba umeme na kuharibu miundombinu ya Shirika.
Aidha
Bw. Kiongo alimuhakikishia Mkuu wa mkoa kuwa wao kama watu wenye
ulemavu ni kama watu wengine, ni mara chache kusikika wasioona ikiwa na
sifa ya kuliibia shirika la umeme na watakuwa mabalozi wa kuhakikisha
Tanesco haiujumiwi ili kukuza kipato chake kwa maendeleo ya Shirika na
Taifa kwa ujumla