mgombea pekee wa nafasi ya uenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani,
Frederick Sumaye ameshindwa kutetea nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura
ya hapana.
Katika uchaguzi huo uliofanyika leo Alhamisi Novemba 28, 2019 mjini
Kibaha Mkoa wa Pwani, Sumaye aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania
mwaka 1995 hadi 2005 amepigiwa kura 28 za ndio na 48 za hapana na kura
moja imeharibika.
Matokeo hayo yametangazwa na msimamizi wa uchaguzi, Patrick Ole Sosopi
ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha).
Akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo, Sumaye amesema lililofanyika ni
demokrasia japo hana uhakika kama kutoa adhabu kwa mtu aliyekuwa
anatumia haki yake kufanya demokrasia ni sahihi.
Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo baadhi ya wajumbe na wanachama
waliokuwepo walilipuka kwa shangwe huku wakiimba nyimbo mbalimbali za
chama.