Picha : agape yaendesha kikao kujadili kutengeneza muongozo wa kupambana na ukatili sokoni shinyanga

Shirika
lisilo la kiserikali Agape Aids Control Programme limeendesha kikao cha
kujadili namna ya kutengeneza muongozo ambao utatumika kwenye masoko ya
Shinyanga Mjini, kwa ajili ya kuzuia na kupambana na ukatili wa
kijinsia kwenye Masoko.

Kikao
hicho kimefanyika leo Novemba 28, 2019, kwenye ukumbi wa mikutano wa
hoteli ya Liga, ambacho kimeshirikisha viongozi wa masoko sita ya
Shinyanga mjini, maofisa ustawi, maendeleo ya jamii, wanasheria, dawati
la jinsia, pamoja na wajumbe wa kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa
wanawake na watoto Mtakuwwa.


Akizungumza
wakati wa kufungua kikao hicho, Mwansheria kutoka Shirika la Agape
Felix Ngaiza, akimwakilisha mkurugenzi wa Shirika hilo John Myola,
amesema, utengenezaji wa muongozo huo wa kuzuia na kupambana na ukatili
kwenye masoko, utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matukio ya ukatili
wa kijinsia masokoni.


Amesema
Shirika hilo limekuwa likitekeleza mradi wa kupambana na matukio ya
ukatili wa kijinisa sokoni, uitwao Mpe Riziki Si Matusi, ambapo sasa
wameamua watengeneze muongozo ambao utatumika kuzuia na kupambana na
matukio hayo ya ukatili wa kijinsia sokoni, ili pawe mahali salama pa
kufanyia biashara.


“Muongozo
huu ni muhimu sana ambao utasaidia kuzuia na kupambana na matukio ya
ukatili wa kijinsia masokoni, na ndio maana leo tumeamua kufanya kikao
na viongozi wa masoko, maofisa ustawi jamii, maendeleo, dawati la
jinsia, wanasheria, na wajumbe wa Mtakuwwa, ili tupate kuutengeneza na
kuanza kutumika,”amesema Ngaiza.



Aidha
amesema muongozo huo wa kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia
kwenye Masoko, utakuwa ukitoa faini na adhabu mbalimbali kwa watu ambao
watakuwa wakifanya matukio hayo ya ukatili kwenye masoko.


Naye Afisa mradi wa kutokomeza ukatili sokoni wa ‘Mpe Riziki Si Matusi’
Helena Daudi, amesema mradi huo umeanza kutekelezwa tangu mwaka Novemba
2018 ambao unakoma mwaka huu 2019, ambapo mpaka sasa wamefanikiwa
kupunguza ukatili huo kwa kiwango kikubwa.


Amesema
mradi huo unafadhiliwa na Shirika la UN WOMEN kupitia shirika la
Equality for Growth (EFG), ambao umedhamiria kutokomeza ukatili kwenye
masoko sita ya manispaa ya Shinyanga dhidi ya wanawake na wasichana,
ambayo ni Kambarage, Soko kuu, Nguzonane, Ngokolo, Majengo mapya, na
Ibinzamata.


Nao
baadhi ya wenyeviti wa masoko akiwemo Alex Stephen kutoka soko kuu la
Shinyanga, wamebainisha matukio ya ukatili ambayo yamekuwa yakitendeka
ikiwamo kutolewa kwa lugha chafu za matusi ya nguoni, kushikwa maumbile
kwa wanawake bila ya ridhaa yao, kutakwa kimapenzi kwa nguvu,
kudhulumiwa pamoja na vipigo.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI


Mwanasheria wa Shirila la Agape Felix Ngaiza akizungumza wakati wa
kufungua kikao cha kujadili namna ya kutengeneza muongozo wa kuzuia na
kupambana na ukatili wa kijinsia sokoni. Picha zote na Marco Maduhu – Malunde 1 blog


Afisa
mradi wa kutokomeza ukatili sokoni wa ‘Mpe Riziki Si Matusi’ kutoka
Shirika la Agape Helena Daudi, akielezea umuhimu wa masoko kuwa na
muongozo huo wa kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia sokoni,
ambapo utasaidia kutokomeza ukatili huo.


Afisa
mradi wa kutokomeza ukatili sokoni wa ‘Mpe Riziki Si Matusi’ kutoka
Shirika la Agape Helena Daudi, akielezea umuhimu wa masoko kuwa na
muongozo huo wa kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia sokoni,
ambapo utasaidia kutokomeza ukatili huo.



Mwanasheria kutoka Shirika la Agape Emmanuel Nyalada akiwasilisha mada
kuhusu muongozo wa kuzuia na kupambana na ukatili kijinsia sokoni.


Meneja miradi kutoka Shirika la Agape Peter Amani, akizungumza kwenye kikao hicho.


Mwanasheria wa manispaa ya Shinyanga Mushi Josephat akieleza kuwa
muongozo huo wa kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia sokoni
utasaidia kumalizana kesi wao kwa wao zinazohusu ukatili, kuliko
kupelekana kwenye vyombo vya Sheria ambapo matukio yote ya ukatili ni
Makosa ya Jinai.



Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha kujadili utengenezaji wa muongozo ambao
utasaidia kuzuia na kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia sokoni.



Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha kujadili utengenezaji wa muongozo
ambao utasaidia kuzuia na kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia
masokoni.



Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha kujadiri utengenezaji wa muongozo ambao
utasaidia kuzuia na kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia
masokoni.


Wajumbe wakiendelea na kikao.

Wajumbe wakiendelea na kikao.

Wajumbe wakiendelea na kikao.

Mwenyekiti wa Soko kuu la Shinyanga Alex Stephen akichangia mada kwenye kikao hicho.

Mhasibu wa Soko la Ibinzamata Juliana Francis akichangia mada kwenye kikao hicho.

Msaidizi wa kisheria kutoka Soko kuu la Shinyanga Zera Semuguruka, akichangia mada kwenye kikao hicho.

Mwakilishi wa Soko la Nguzo Nane Hilda Athanas, akichangia mada kwenye kikao.

Mchungaji wa kanisa la KKKT Makedonia Harold Mkaro, ambaye pia ni mjumbe wa MTAKUWWA, akichangia mada kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kazi ya makundi.