Breaking : rais magufuli amsimamisha kazi rpc ,rco na meneja wa tra mkoa wa shinyanga

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli amewasimamisha kazi Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP
Richard Ambwao na Mkuu wa Upelelezi RCO wa Mkoa wa Shinyanga SSP John
Rwamulema kupisha uchunguzi wa tuhuma za kushirikiana na wamiliki wa
kiwanda cha pombe kukwepa kodi.


Wawili hao wamesimamishwa kazi wakidaiwa
kushirikiana na wamiliki wa kiwanda cha kutengeneza pombe kali cha
Canon cha mkoani Shinyanga kukwepa kodi.

“Sababu ya pili ni utovu wa nidhamu kwa
kushindwa kutekeleza maelekezo waliyopewa na mwenyekiti wa kamati ya
ulinzi na usalama ya Mkoa wa Shinyanga ambaye ni mkuu wa Mkoa huo,
Zainab Telack,” inaeleza taarifa hiyo.