Meja Jenarali Mstaafu Hamisi Semfuko akikagua gwaride la wahitimu wa mafunzo ya Jeshi Usu
Baadhi ya wahitimu wakionyesha mbinu mojawapo ya kukabiliana na adui bila silaha
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
mkoa wa Katavi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi katika
mafunzo hayo Meja Jenerali Mstaafu Hamisi Semfuko.

Mwenyekiti wa
bodi ya mamlaka ya Uhifadhi Wanyama Pori Nchini (TAWA) Meja Jenerali
Mstaafu Hamisi Semfuko amesema mfumo wa mafunzo ya Jeshi Usu
yanayobadili watumishi wa Wizara ya Mali asili kutoka katika hali ya
uraia wa kawaida na kuwa askari yameleta mafanikio makubwa tangu
kuanzishwa kwake miaka minne iliyopita

Amesema hayo wakati akifunga mafunzo hayo kwa wahitimu 535 katika Kituo cha Mafunzo Mlele mkoani Katavi
Aidha amewataka
wahitimu hao kuishi yale waliyojifunza chuoni hapokwa kipindi cha miezi
mitatu katika kuhakikisha Tanzania inatokomeza kabisa matukio ya
ujangili yanayofanyika katika hifadhi na mapori mbalimbali hapa nchini

Kwa upande wao
baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo wameyasifu kwa kuwajengea ukakamau na
kuwapa mbinumbalimbali za namna ya kukabiliana na adui

“Mbali na taaluma
yangu ya uuguzi hapa nimeongezewa ujuzi ambapo sasa ninaweza kujumuika
na askari katika doria na nikafanya nao kazi vizuri” alisema Ester Myaho
ambaye ni mtumishi kutoka Wizara ya Mali Asili na Utalii

Pia wameiomba
serikali kuboresha mazingira ya chuo hicho kwani kinakabiliwa na
changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa jiko la kupikia chakula cha
wanafunzi na bwalo la chakula pamoja na ukosefu mitandao ya simu za
mkononi

Wahitimu hao wamepata mafunzo kadhaa ikiwemo namna ya kutumia silaha na kareti
Awali akizungumza
kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Katavi, Mkuu wa wilaya ya Mpanda Lililan
Matinga alisema mkoa wa Katavi unashirikiana na Wizara ya Mali Asili na
Utalii katika kulinda mali asili