Rc tabora awataka wasimamizi wa uchaguzi kuchukua tahadhiri ya mvua ili kuepuka uchaguzi ujao kuathiriwa

Mkuu wa Mkoa wa Tabora
Aggrey Mwanri (mwenye koti jeusi) akiwa ndani ya Kituo cha Kura cha
Ilolangulu  akitoa maelelekezo maalumu  leo kwa Viongozi wa Wilaya ya
Uyui wakati alipoongoza Kamati ya Usalama Mkoa wa Tabora kukagua Vituo
vya Upigaji kura za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa siku ya Jumapili ijayo
ili kujiridhisha maandalizi kama yanakwenda vizuri.
Mkuu wa Wilaya ya
Nzega Godfrey Ngupula akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey
Mwanri (mwenye tshirt yenye mistari ) na Wajumbe wa Kamati ya Usalama
Mkoa wa Tabora jinsi walivyojipanga kuhakikisha wapigaji kura maeneo ya
wazi watakavyoshiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa wakati Kamati hiyo
ilipokwenda kukagua Vituo vya Upigaji kura za Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa siku ya Jumapili ijayo ili kujiridhisha maandalizi kama yanakwenda
vizuri.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora
Aggrey Mwanri (mwenye koti jeusi) akiwa nje  ya Kituo cha Kura cha
Ilolangulu  akitoa maelekezo maalumu   kwa Viongozi wa Wilaya ya Uyui
wakati alipoongoza Kamati ya Usalama Mkoa wa Tabora kukagua Vituo vya
Upigaji kura za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa siku ya Jumapili ijayo ili
kujiridhisha maandalizi kama yanakwenda vizuri.
WAKATI Mvua zimeanza kunyesha
katika maeneo mbalimbali ,Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri
amewaagiza Wasimamizi wa Uchaguzi wote mkoani humo kuhakikisha
wanachukua tahadhari kwa kujenga na kuimarisha Vituo vya Kupigia Kura
vilivyopo katika maeneo ya wazi kama vile kwenye miti kwa kuweka
Maturubai mapema.
Hatua hiyo inalena kuhakikisha kuwa zoezi la upigaji kura la jumapili ijayo ariathiriwa na maji ya mvua.
Mwanri alitoa kauli hiyo jana
wakati wa ziara yake na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Uslama ya Mkoa na
ile ya Wilaya ya Nzega , Uyui na Igunga wakati wa kukagua maandalizi ya
maeneo ya kupigia kura Jumapili ijayo.
Alisema ni vema Vituo ambavyo
vimepangwa katika maeneo ya wazi vikajengwa mapema kwa kutumia Maturubai
katika eneo ambalo wananchi watakapotumia kupiga kura na eneo ambalo
Mawakala wa Vyama vya Siasa watakapokaa.
Mwanri alisema pia lazima kuwepo
eneo ambalo wananachi wanaosubiri kupiga kura wanaweza kujihifadhi
endapo mvua itanyesha siku ya uchaguzi.
“Pamoja na kuwa Vituo vya wazi
havipo katika majengo na kama  mnapanga kujenga Mahema basi wekeni
mazingira mazuri ya watu wanaokuja kupiga kura ili wawe na uhakika hata
kama mvua ikinyesha ghafla , hatanyeshewa na vifaa vya kupiga kura
havitaathirika na mvua” alisisitiza.
Alisema sanjari hilo amewataka
Wasimamizi hao kuhakikisha kuwa vifaa vyote vya kuendesha zoezi la
uchaguzi vinafika mapema katika eneo la tukio ili kuhakikisha zoezi
linakwenda kwa kwa wakati uliopangwa na hakuna wananchi watakaokosa
kupiga kura kwa sababu ya ukosefu wa vifaa hivyo.
Kwa upande wa Kaimu Katibu Tawala
Mkoa wa Tabora Rukia Manduta aliwataka Wasimamizi wa Uchaguzi
kuhakikisha kuwa maeneo ambayo watajenga na kuweka Maturubai kuwa kwenye
miununoko.
Alisema hatua hiyo itazuia kuharibika vifaa ikiwemo karatasi za kupigia kura kutokana na maji ya mvua
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Selemani Sikieti alisema tayari
wameshanunua Maturubai kwa ajili ya kutekeleza zoezi hilo na watachukua
tahadhari zote ili kufanya zoezi la upigaji kura kukamilika bila vikwazo