Maaskofu mwanza wachekelea kanisa la mfalme zumaradi kufungwa…wataka serikali ikomae zaidi

Mkuu wa Wilaya Nyamagana alipofanya ziara kwenye Kanisa la Mfalme Zumaradi.
Viongozi wa Umoja wa Makanisa (UMJM), jijini Mwanza, unaoundwa na
Mabaraza matatu ya TEC, CCT na CPCT, umeitaka Serikali kuyapitia upya
Makanisa mengine ambayo usajili wake haueleweki, ili kuondoa sintofahamu
kwa waumini wa madhehebu hayo.
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku chache baada ya Kamati ya ulinzi na
Usalama Wilaya ya Nyamagana, ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya Dkt. Philis
Nyimbi, kufungia Kanisa la Mfalme Zumaridi lililopo eneo la Iseni jijini
humo ambalo linadaiwa kuendesha Ibada zake kinyume cha sheria na Katiba
ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, Mwenyekiti wa umoja
huo, Askofu Philipo Mafuja amesema hatua hiyo iliyofanywa na viongozi wa
Serikali kuyafungia Makanisa yanayoendeshwa kinyume cha sheria
yanabaraka hata kwa Mungu.
“Maandiko matakatifu yanasema tuilinde imani na kulinda imani ni hii
kuyachukulia hatua baadhi ya Makanisa ambayo yanafanya kazi kinyume na
utaratibu” amesema Askofu Philipo Mafuja
Novemba 18, 2019 Uongozi wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza umepiga
marufuku ibada zinazoendeshwa na kiongozi wa kanisa la Mfalme Zumaridi
hadi hapo Serikali itakapojiridhisha kuwa ibada hazikinzani na sheria za
nchi.