Tetesi za soka ulaya jumatano 20.11.2019: sterling, pochettino, terry, haaland, moreno

SterlingManchester City imeanza mazungumzo kuhusu mkataba mpya na mshambuliaji wa kimataifa wa England Raheem Sterling, 24. (Mirror)

Mkufunzi
wa Leipzig, Julian Nagelsmann na Jose Mourinho wanapigiwa upatu
kuchukua nafasi ya Mauricio Pochettino, aliyefutwa kazi kama mkufunzi wa
Tottenham. (Star)

Wengine ambao wamejumuishwa katika orodha hiyo
ni Eddie Howe wa Bournemouth na Carlo Ancelotti wa Napoli ambao huenda
wakapata kazi katika uwanja wa Tottenham Hotspur. (Sun)

Fidia itakayolipwa na Tottenham kwa kumfuta Pochettino na wafanyikazi
wake huenda ikafikia £19.6m kiwango ambacho Manchester United ilimlipa
Jose Mourinho na timu yake mwezi Disemba 2018. (Mirror)
 Jose Mourinho alikuwa mkufunzi wa Manchester United kwa miaka miwili na nusu kabla ya kupigwa kalamu Disemba 2018
Pochettino
alifutwa kazi kufuatia malumbano kati yake na wachezaji katika chumba
cha kubadilisha nguo hali ambayo ilifikia kiwango cha kuathiri
utendakazi wake. (Mail)

Pochettino
alikataa ombi la Daniel Levy la kumtaka ajiondoe hatua ambayo
ilimfanya mwenyekiti wa Spurs chairman kumfuta kazi siku ya Jumanne.
(Telegraph)

Red Devils huenda wakalipa hadi £85m kumsaini
mshambuliaji wa Salzburg na Norway mzaliwa wa Leeds-Erling Braut
Haaland, 19. (Standard)

Manchester United inamfuatilia mshambuliaji wa Reading Danny Loader,
19, ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu. (Mirror)

 Sergio Aguero
Nahodha
wa zamani wa Chelsea John Terry, amepuuzilia mbali tetesi kuwa alitoa
wito kwa Blues kutomsajili mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero kabla
ahamie Manchester City. (Mirror)

Swansea na Stoke zinamtaka winga wa Celtic wa miaka 32- Jonny Hayes mkataba wake unapoelekea kukamilika. (Scottish Sun)

Robert Moreno anatarajiwa kutoa kauli yake kuhusu hatma yake kama
kocha wa Uhispania baada ya hatua ya mkataba wake kuvunjwa. (AS – in
Spanish)

Wachezaji wa Manchester United wameombwa kutotoka nje kwa
zaidi ya dakika kumi watakaposafiri kucheza na FC Astana katika ligi
ya Europa kutokana na hali ya baridi kali nchini Kazakhstan. (ESPN)