Sima atoa agizo kituo cha kupokea gesi asilia cha songas kuwasilisha mpango kazi wa usimamizi mazingira

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (kulia) akiwasili katika
kituo cha kupokea gesi asilia cha Songas eneo la Somanga Wilaya ya Kilwa
mkoani Lindi kwa ajili ya kukagua na kupokea taarifaya madhara
yaliyotokana na kuvuka kwa nishati hiyo. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya
ya Kilwa Christopher Ngubiagai.
Meneja wa kituo cha kupokea gesi
asilia cha Songas Salehe Kifunga (aliyesimama mwenye shati jeupe) akitoa
maelezo kuhusu kituo hicho kinavyofanya kazi kwa Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima aliyeambatana na
viongozi wengine.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (kulia) akizungumza wakati
wa ziara katika kituo cha kupokea gesi asilia cha Songas eneo la Somanga
Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (kulia) akitoa maelekezo
baada ya kukagua kituo cha kupokea gesi asilia cha Songas.
Eneo la kituo cha Songas kama
linavyoonekana wakati wa ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima pamoja na viongozi wa Baraza la
Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC).
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa
Christopher Ngubiagai akizungumzia kuhusu tukio la kuvuja kwa gesi
lilivyotokea mbele ya viongozi mbalimbali wakati wa ziara hiyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (kulia) akijadili jambo na
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai mara baada ya kukagua
kituo cha Songas.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (kulia) akiagana na Mkuu wa
Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai mara baada ya kukagua kituo cha
Songas.
…………….
Na Robert Hokororo, Kilwa
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima ameagiza kituo cha kupokea
gesi asilia cha Songas eneo la Somanga kuwasilisha mpango kazi wa
usimamizi wa mazingira unaoonesha madhara na hatua zinazochukuliwa pindi
yanapotokea maafa.
Sima ametoa agizo hilo leo wakati
wa ziara yake akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa
la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Prof. Esnath Chagu na
Mkurugenzi Mkuu Dkt. Samuel Gwamaka kukagua kituo hicho ambacho Novemba 3
mwaka huu kilipata tatizo la kuvujisha bomba la mafuta katika eneo hilo
wilayani Kilwa mkoani Mtwara.
Katika ziara hiyo inayohusisha
mikoa ya Lindi na Mtwara alisema kuwa ni muhimu wananchi wa vijiji zaidi
ya 60 vilivyopitiwa na mradi wa bomba la gesi asilia licha ya kujua
faida zake lakini pia wanatakiwa wapate elimu sahihi ya madhara pindi
yanapotokea matatizo kama haya.
Aidha, Naibu Waziri huyo aliongeza
kuwa nchi yetu imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi na hasa ya gesi
asilia na kutaka mikataba ambayo inaingia na wakandarasi lazima ioneshe
wananchi wameshirikishwaje na kuelewa kuhusu madhara yatakajitokeza
endapo gesi itavuja.
Alisema kuwa lazima kama nchi
tujuie mikataba hii ili kama yakitokea maafa wao wanawajibikaje kutokana
na madhara yanayoweza kujitokeza hususana kwa wananchi wanaopitiwa na
miradi hiyo.
“Tumekuja hapa tuone kama mkiradi
hii inafuata sheria ya mazingira yam waka 2004 na hapa tunataka tuone
kwenye eneo hili yakitokea madhara ni hatua gani zinachukuliwa, tunataka
kuona taarifa kamili na tuangalie kwenye eneo letu la mazingira
mnachukua hatua gani.
“Hebu turudi kuangalia mkataba huu
makubaliano gani tunawekeana sio valvu mpya imetoka maabara imekuja
ikawekwa hapa halafu ikajivusha gesi, hapana lazima tuje na majibu
sahihi. Natambua wizara husika imefanya kazi yao na sisi tunaoratibu
shughuli za mzingira lazima tufanye kazi yetu,” alisema Sima.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi
ya NEMC) Prof. Chagu alisema ni muhimu kwa watalamu kuhakikisha vifaa
vinavyototumika vinakuwa na viwango.
Prof. Chagu alisema kuwa matumizi
ya vifaa vyenye viwango yatasaidia katika kuhakikisha matatizo kama haya
hayatokei na kuleta madhara kwa wananchi na hata kama yakitokea basi
lazima tujue hatua za kuchukua. 
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Kilwa Christopher Ngubiagai alisema hili ni tukio baya kutokea na kama
wasingekuwa makini kuzuia cheche ingekuwa hali ya hatari na kusababisha
maafa makubwa. 
Ngubiaga alibainisha kuwa katika
siku ya tukio hilo wananchi wanaotumia Barabara ya Kilwa hususan
wasafiri wa mabasi ya kwenda au kutoka Mtwara na Songea waliathirika
kutokana na kutoendelea na safari.
Pia alisema kuwa athari za
kiuchumi zilionekana kutokana kuzimwa kwa kituo cha umeme Kilwa kutoka
muda wa jioni hadi usiku hivyo wananchi walikosa huduma hiyo na
kushindwa kufanya shughuli za kiuchumi.