Mratibu wa mradi wa ‘ Mfuko wa Canada
kwa ajili ya mipango ya kijamii’ kutoka Shirika la Under The Same Sun,
Grace Wabanhu akitambulisha mradi huo kwa wanawake wenye ualbino na wanawake wenye watoto wenye ualbino katika mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Shirika la Under The Same Sun
limetambulisha rasmi mradi wa ‘ Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya
kijamii – Canadian Fund For Local Initiative(CFLI)’ wenye lengo la
kuwajengea uwezo wanawake wenye ualbino na wanawake wenye watoto wenye
ualbino katika mkoa wa Shinyanga kuhusu ualbino ili wawe na uelewa wa
kutosha na kupata ujasiri wa kuielimisha jamii juu ya hali ya ualbino.

Mradi huo umetambulishwa leo Jumatatu
Novemba 18,2019 katika ukumbi wa Shinyanga Fairies Hotel Mjini Shinyanga
wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu kuhusu elimu ya ualbino kwa
na wanawake wenye ualbino na wanawake wenye watoto wenye ualbino 30
kutoka wilaya za mkoa wa Shinyanga.
Novemba 18,2019 katika ukumbi wa Shinyanga Fairies Hotel Mjini Shinyanga
wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu kuhusu elimu ya ualbino kwa
na wanawake wenye ualbino na wanawake wenye watoto wenye ualbino 30
kutoka wilaya za mkoa wa Shinyanga.
Mratibu wa mradi wa ‘ Mfuko wa Canada
kwa ajili ya mipango ya kijamii’ kutoka Shirika la Under The Same Sun,
Grace Wabanhu alisema mradi huo wa miezi minne unaotekelezwa katika mkoa
wa Shinyanga na Mwanza utafikia tamati mwezi Januari,2020.

“Lengo la mradi unaofadhiliwa na watu wa
Canada ni kutoa elimu ya ualbino kwa wanawake hawa,tumechukua wanawake
30 kutoka wilaya zote za mkoa wa Shinyanga,Mwanza hivyo hivyo wanawake
30. Wanawake hawa watapata mafunzo ya uelewa juu ya ualbino na wao ndiyo
watakuwa wakufunzi kuielimisha jamii”,alisema.

“Tunatarajia kwamba wanawake
watakaojengewa uwezo watakuwa na uelewa wa kutosha juu ya hali ya
ualbino na watakuwa na ujasiri wa kuielimisha jamii inayowazunguka kwa
lengo la kuondoa unyanyapaa na ukatili dhidi yao na watoto wenye ualbino
ili kuleta usawa kati ya watu wenye ualbino na wasio na
ualbino”,aliongeza Wabanhu.

Alisema wameamua kuchagua kundi la
wanawake wenye ualbino na wanawake wenye watoto wenye ualbino kutokana
na kwamba kundi hilo limesahaulika lakini kwa kuzingatia kuwa akina mama
hao ndiyo wanalea watoto na ni waathirika wakubwa wa vitendo vya
unyanyapaa na ukatili na wamekuwa wakikimbiwa na waume zao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha
Watu wenye ualbino mkoa wa Shinyanga (TAS),Eunice Zabron alisema njia
pekee ya kukomesha vitendo vya unyanyapaa na ukatili dhidi ya watu wenye
ualbino ni kutoa elimu ya kutosha kwa jamii.

Zabron ambaye pia Mwenyekiti wa Idara na
Wanawake na Watoto katika Chama cha Watu wenye ualbino mkoa wa
Shinyanga aliipongeza serikali kwa kuendelea kuwa bega kwa bega na watu
wenye ualbino huku akibainisha kuwa vitendo vya unyanyapaa vimeendea
kupungua kutokana na elimu inayotolewa na vyombo vya habari na wadau
mbalimbali kuhusu ualbino.

Kwa upande wake,Afisa Maendeleo Ustawi
wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Lilian Kiyenze kwa niaba ya
Afisa Maendeleo Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga aliwataka wanawake hao
kutumia vizuri elimu watakayopatiwa kuhusu Ualbino ili wakawe chachu ya
mabadiliko katika jamii.

ANGALIA PICHA
Afisa Maendeleo Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Lilian Kiyenze akizungumza kwa niaba ya Afisa Maendeleo Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga wakati Shirika la Under The Same Sun likitambulisha mradi
wa ‘ Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund
For Local Initiative(CFLI)’ leo Jumatatu Novemba 18,2019. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Afisa Maendeleo Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Lilian Kiyenze akizungumza wakati wa kutambulisha mradi wa Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative(CFLI)’.
Mratibu wa mradi wa ‘ Mfuko wa Canada
kwa ajili ya mipango ya kijamii’ kutoka Shirika la Under The Same Sun,
Grace Wabanhu akitambulisha mradi wa Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative(CFLI)’kwa wanawake wenye ualbino na wanawake wenye watoto wenye ualbino katika mkoa wa Shinyanga.

Mratibu wa mradi wa ‘ Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii’ Grace Wabanhu akielezea kuhusu mradi wa Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative (CFLI).
Grace Wabanhu akizungumza wakati akitambulisha mradi wa Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative(CFLI)’
Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye ualbino mkoa wa Shinyanga (TAS),Eunice Zabron akizungumza wakati wa kutambulisha mradi wa Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative (CFLI).
Wanawake wenye watoto wenye ualbino wakiwa ukumbini wakati mradi wa Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative (CFLI) ukitambulishwa.
Akina mama wakiteta jambo ukumbini.
Wanawake wenye ualbino wakiwa ukumbini wakati mradi wa Mfuko
wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local
Initiative (CFLI) ukitambulishwa rasmi mkoani Shinyanga.

Wadau wakiwa ukumbini wakati mradi wa Mfuko wa Canada kwa ajili ya mipango ya kijamii – Canadian Fund For Local Initiative (CFLI) ukitambulishwa.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog