Mwanafunzi
wa mwaka wa tatu katika Chuo cha Ufundi Trade Peramiho wilayani Songea,
Grayson Maselin (23), amejeruhiwa na mwanafunzi mwenzake Mosses Ngole
(23), kwa kuchomwa kisu shingoni baada ya kummwagia maji machafu siku ya
kumbukizi ya kuzaliwa kwake (birthday).

Ngole,
mwanafunzi wa mwaka wa nne katika chuo hicho, anadaiwa kumchoma kisu
shingoni mwanafunzi mwenzake huyo na kumsababishia jeraha na kuvuja damu
nyingi kwenye sherehe hiyo.

Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa, alidai tukio hilo lilitokea
Jumatano majira ya saa saba mchana katika chuo hicho.

Alidai
kuwa, siku ya tukio, Ngole alikuwa analazimishwa kumwagiwa maji na
kupakwa matope na wanafunzi wenzake ndipo alipopandisha hasira na
kufikia uamuzi wa kumchoma kisu mwanafunzi mwenzake huyo.

Maigwa alidai mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za
kumjeruhi mwanafunzi mwenzake, ambaye kwa sasa amelazwa Hospitali ya
Kanisa Peramiho.