Mahakama yaamuru wabunge wanne wa chadema kukamatwa

 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo
Ijumaa Novemba 15, 2019 imeamuru wabunge wanne wa Chadema kukamatwa kwa
kukiuka masharti ya dhamana.


Wabunge hao na majimbo yao kwenye mabano
ni John Heche (Tarime Vijijini), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini),
Halima Mdee (Kawe) na Ester Bulaya (Bunda).

Amri hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi
Mkuu, Thomas Simba baada ya wabunge hao kutokuwepo mahakamani bila
taarifa yoyote. Hata wadhamini wao pia hawakuwepo.

Pia, Hakimu Simba ametoa hati ya wito wa wadhamini wa wabunge hao kujua sababu za kutowapeleka washtakiwa mahakamani.

Kabla ya kutoa amri hizo, Hakimu Simba
amesema leo kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa,
washtakiwa wengine waliwahi lakini wabunge hao wanne hadi saa 4:05
asubuhi walikuwa hawajafika mahakamani bila sababu za msingi.

Baada ya Hakimu Simba kueleza hayo
wakili wa upande wa utetezi, Faraji Mangula aliyewawakilisha mawakili
Profesa Abdallah Safari, Peter Kibatala na Jeremiah Mtobesya ameieleza
mahakama hiyo kuwa ana taarifa za Bulaya.