Moto wa ajabu waunguza nyumba…paa lateketea bila kuunguza vitu ndani

Habari zilizotufikia hivi punde kutoka
shehia ya Maziwani wilaya ya Wete Pemba, na kuthibitishwa na sheha wa
shehia hiyo, zinaeleza kuwa, kuna nyumba imeungua moto sehemu ya mapaa
tu, ambapo moto huo uliopewa jina la moto wa maajabu, haukuunguza vitu
vingine.

Aidha moto huo haukugharimu maisha ya
mtu yeyote, pamoja na paa kuteketea lote, lakini hakuna kitu chengine
kilichoathirika kutokana na moto huo.