Mipango mkakati dhidi ya wafugaji wazinduliwa arusha


Na Mwandishi wetu APC BLOG, ARUSHA
Mkuu wa mkoa wa Arusha
mrisho  amezindua mpango mkakati wa  kibiashara wa wilaya mbili za
simanjiro  na longido ambao unalenga  kuweka mipango ya namna  gani 
wafugaji watajikwamua kiuchumi.
Akizungunza katika
warsha ya uzinduzi wa mpango huo uliofadhiliwa na  mradi wa Maisha bora 
kwa ushirikiano wa shirika la Trias Gambo amesema kuwa mpango huo
utawezesha wafugaji wa wilaya hizo kuwa na thamani  hapa nchini.
Amesema kuwa kupitia
mpango huo uliozinduliwa wafugaji wanapaswa kuongeza mnyororo wa 
thamani ya mifugo yao ili waweze kuzalisha kwa tija na kwa faida tofauti
na walivyozoea kufuga kimazoea.
Aidha ameishukuru
serikali  ya Beljam kwa kutoa kiasi cha dola za kimarekani milioni 11
kuhakikisha mradi huo unatekelezeka katika wilaya za longido na
simanjiro.
Nae mkurugenzi wa
shirika la Trias  afrika mashariki bw Bart Casier  amesema kuwa wameamua
kushirikiana na serikali ili kuwakwamua kiuchumi wafugaji katika
kuhakikisha wanaondokana na changamoto zinazowakabili.
Amesema kuwa mbali na
kusaidia miradi hiyo hadi sasa wamefainikiwa kusaidia vikundi vya vikoba
450  kwa kuwakopesha  pamoja na vyama vya kuweka na kukopa  (sacos)
lengo likiwa ni kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.
Amesema kuwa wanafanya
kazi kwa kushirikiana na serikali pamoja na sekta nyingine ili kukomboa
jamii kwenye sekta za biashara,lishe,maji pamoja na mitaji.
Kwa  upande wake mkuu wa
wikaya ya longido frenk Mwaisumbe amewashukuru maisha  bora  kwa
kushirikiana na serikali kwa kuwawezesha mradi huo kwani anaamini
utawanufaisha wafugaji lakini pia kuwanufaisha wanawake kwa kuwapatia
mikopo.
Mwaisumbe alimalizia kwa
kusema kuwa bado katika jamii   za wafugaji kunawanaofuga kama
utamaduni hali ambayo inasababisha washindwe kufikia malengo yao lakini
sasa kupitia mkakati  huo hali itabadilika