Na Mwandishi wetu, Dar es salaam
Serikali imeitaka Taasisi ya UONGOZI (UONGOZI
Institute) kutoa mafunzo ya ungozi kwa viongozi mbalimbali wa Serikali
katika maeneo yao kazi ili kuiwezesha Serikali kufikia lengo la kuimarisha
utawala bora, badala ya kusubiri viongozi hao kufuata huduma mafunzo katika ofisi
za taasisi hiyo zilizopo jijini Dar es Salaam.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb)
wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watendaji wa taasisi hiyo,
kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam
jana kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, kuwapelekea mafunzo viongozi
wa Serikali katika maeneo yao ya kazi kutapunguza gharama kubwa zinazotumika
kuwasafirisha viongozi hao kwenda jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata semina
elekezi na mafunzo mbalimbali ya uongozi yanayotolewa na taasisi hiyo.

Dkt. Mwanjelwa amefafanua kuwa, mafunzo ya viongozi
yakitolewa mahala pa kazi yatasaidia kuharakisha utoaji wa elimu ya maadili kwa
viongozi wa umma, hivyo taasisi hiyo itakuwa na mchango mkubwa katika kuwezesha
kuifikia azma ya Serikali ya kuwa na viongozi waadilifu.

Sanjali na hilo, Dkt. Mwanjelwa
ameitaka Taasisi ya UONGOZI kuhakikisha inatoa elimu ya umuhimu wa viongozi katika
Taasisi zote Umma nchini kufanya kazi kwa ushirikiano kama timu ili kuongeza
ufanisi wa utendaji kazi.

Aidha, Dkt. Mwanjelwa ameishauri taasisi hiyo kuhakikisha
inawasilisha Serikalini wazo lao la kuanzisha Kituo cha Tathmini ya Viongozi
kwani kituo hicho kitakuwa ni msaada mkubwa kwa viongozi kutambua maeneo ambayo
hawafanyi vizuri kiutendaji na kuyaboresha na kwa yale wanayofanya vizuri
kiutendaji kuyaendeleza.

Naye, Mkuu wa Idara ya Mafunzo kwa Viongozi wa Taasisi ya
UONGOZI, Bw. Kadari Singo amesema, Taasisi hiyo imeshatoa mafunzo elekezi kwa
viongozi mbalimbali nchini kwa vipindi tofauti licha ya kuwepo kwa changamoto ya
baadhi ya viongozi kutomaliza mafunzo yao na wengine wanapomaliza hatua ya
mwanzo hawaendelei na hatua inayofuata kwa mujibu wa taratibu ya mafunzo husika.

Pamoja na kuwepo kwa changamoto hiyo, Bw. Singo hakusita
kuishauri Serikali kuendelea kuweka msisitizo wa kutoa mafunzo kwa viongozi wanaoteuliwa
ili kuwajengea uwezo kiutendaji utakaowawezesha kutekeleza majukumu yao
kikamilifu.

“Taasisi ya UONGOZI inaishauri
Serikali kuwa na utaratibu endelevu wa kutoa mafunzo kwa viongozi kabla ya
kupandishwa vyeo, na iendelee kusisitiza utoaji wa mafunzo elekezi kwa viongozi
wanaoteuliwa ili kuwajengea uelewa wa namna Serikali inavyofanya kazi, ikiwa ni pamoja
na kuwapatia fursa ya kufahamu vipaumbele
vya Serikali na miiko ya Utumishi wa Umma’’, Bw. Singo amesisitiza.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya
UONGOZI Prof. Joseph Semboja amemshukuru Dkt. Mwanjelwa kwa kufanya ziara ya
kikazi kuhimiza uwajibikaji katika Taasisi yake na kumhakikishia kuwa, taasisi
yake itafanyia kazi maelekezo na ushauri alioutoa kwa lengo la kuongeza ufanisi
wa utendaji kazi katika Taasisi hiyo.

Ziara hiyo ya kikazi ya Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb)
katika Taasisi ya UONGOZI ni mwendelezo wa utekelezaji wa majukumu yake ya
kusimamia na kuhimiza uwajibikaji wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.