Mfumuko wa bei wa taifa waongezeka hadi asilimia 3.6 % kutoka asilimia 3.4

Na: Mwandishi Wetu, MAELEZO -Dodoma

Mfumuko
wa bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unaoishia mwezi Oktoba 2019
umeongezeka hadi asilimia 3.6 kutoka asilimia 3.4 mwaka ulioishia mwezi
Septemba 2019 ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.2. 

Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari kutangaza takwimu za bei, Kaimu
Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu, Bibi. Ruth Minja
amesema kuwa ongezeko hilo limetokana na kasi ya bei za bidhaa na huduma
kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2019 imeongezeka ikilinganishwa na
kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba2019. 
Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 115.84 mwezi Oktoba, 2019 kutoka 111.83 mwezi Oktoba, 209 
“Ongezeko
hili la mfumuko wa bei limetokana na ongezeko la bei za bidhaa za
Vyakula na Vinywaji Baridi  ambapo mfumuko wa bei kwa mwezi Oktoba, 2019
umeongezeka hadi asilimia 5.1 toka asilimia 4.0 mwezi Septemba, 2019.”
Alisema Bibi. Ruth. 
Aidha
amesema kuwa mfumuko wa bei kwa bidhaa na huduma zote ambazo
hazijumuishi chakula na nishati kwa mwezi Oktoba, 2019 umepungua kidogo
hadi asilimia 2.6 kutoka asilimia 2.6 kutoka  asilimia 2.7 Septemba,
2019 
Fahirisi
za Bei kati ya mwezi Septemba, 2019 na mwezi Oktoba, 2019 zimepungua
kwa asilimia 0.1 ambapo badiliko ni sawa na badiliko lilivyokuwa kati ya
mwezi Agosti, 2019 na mwezi Septemba 2019 
Alizitaja
baadhi ya bidhaa zilizochangia kupungua kwa fahirishi kuwa ni pamoja na
mafuta ya taa kwa asilimia 2.5, dieseli kwa asilimia 2.1, petrol kwa
asilimia 4.0. vifaa kwa ajili ya uchakataji wa taarifa kama kompyuta kwa
asilimia 5.1 na baadhi ya huduma binafsi. 
Tanzania
kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ambayo ndiyo mamlaka ya
kutangaza takwimu pamoja na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki imekuwa na utaratibu wa kutangaza matokeo ya mfumuko wa bei 
kila mwezi ambapo ambapo mfumuko wa bei katika nchi hizo utangazwa.