Dc same atangaza vita na majangili wanaoua wanyama kwenye hifadhi

MKUU
wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Rosemary Sitaki ametangaza vita
mpya na majangili wanaoingia kwenye hifadhi na kuua wanyama kwamba
hawatapata nafasi kutokana namna serikali ilivyojipanga kukabiliana nao
huku akieleza watakaokamatwa watashughulikiwa kwa hatua kali za
kisheria.
Pia
amewataka wabadilishe biashara hiyo na sasa waanza kujikita kwenye
kufanya ujenzi wa hoteli za kitalii ili waweze kujiingizia kipato badala
ya kufikiria kuendelea kufanya vitendo vya ujangili kwenye hifadhi.
DC
Sitaki aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu
namna kama serikali walivyojipanga kuhakikisha wanapambana na vitendo
vya ujangili vilivyopo kwenye maeneo yao ambapo alisema watu hao hawana
nafasi kwenye wilaya hiyo.

“Labda
tu niwaambie kwamba hifadhi zote zina askari nikihesabu majeshi yote
niliyokuwa nayo hatutawapa nafasi kwani serikali wamejipanga na ukienda
kwenye hifadhi zote ni askari kwa maana ya kuzuia watu wasiingie na
kuuwa wanyama na kuharibu mazingira hivyo na ambao watasubutu kufanya
hivyo tutawachukua hatua kali kama tukikuta mvua anadhamira mbaya na
hifadhi zetu tumesimama imara tunataka vivutio hivyo vizazi vya sasa na
na vijavyo vivikute”Alisema DC Sitaki.
Alisema
kwamba kasi ya serikali ni kuhakikisha inafanya utalii unakuwa sehemu
ya kiuungia mapato kwenye nchi hivyo wo hawawezi kufanya uzembe ambao
utafanya vivutio hivyo kupunguza hadhi yake  au kupunguza sifa yake
ikiwemo wanyama na kuharibu mazingira.
Hata
hivyo alisema kwamba hivi sasa wanafuatilia maeneo ambayo wanyama
walikuwa wanapita waone kama maeneo hayo yameendeleza kiasi gani au
hayaendelezwa kama hayajaendelezwa yaachwe wazi kusiwe na muingiliano
kati ya shughuli za binadamu na wanyama ili kuona namna ya kufanya ili
kuondoa hali hiyo.
Akizungumzia
suala la wafugaji kuingia mifugo kwenye hifadhi hiyo Mkuu huyo wa
wilaya anasema kwamba changamoto hiyo ilikuwa ni kubwa ilikuwa
inawasumbua sana lakini miaka ya hivi karibuni kutokana na juhudi kubwa
za kusimamia sheria na kutoa elimu kwa wafugaji mifugo idadi ya mifugo
inayoingia ngombe na mbuzi wanaoingia kwenye hifadhi hiyo.