Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya
Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhandisi Styden Rwebangila akizungumza
wakati wa kikao baina ya Kamati hiyo, wataalamu wa TANESCO, REA na
mwakilishi wa Mkandarasi anayetekeleza miradi ya umeme vijijini mkoani
Mtwara (hawapo pichani), Oktoba 31, 2019.

Wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya
Bodi ya Nishati Vijijini (REB) wakikagua utekelezaji wa miradi ya umeme
vijijini katika kijiji cha Maili Sita, Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara,
Oktoba 30, 2019.

Kamati ya Ufundi ya Bodi ya
Nishati Vijijini (REB) wakiwa katika kikao na wataalamu wa TANESCO, REA
na mwakilishi wa Mkandarasi anayetekeleza miradi ya umeme vijijini
mkoani Mtwara, Oktoba 31, 2019. Kamati ilikuwa katika ziara kukagua
utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.

Veronica Simba – Mtwara
Bodi ya Nishati Vijijini (REB)
imeweka kusudio la kufuta mkataba mmojawapo wa mkandarasi anayetekeleza
miradi ya umeme vijijini mkoani Mtwara na sehemu ya Mkoa wa Tanga,
ambaye ni muunganiko (JV) wa kampuni za Radi Services Ltd, Njarita
Contractors Ltd & Aguila Contractors Ltd.

Kusudio hilo liliwekwa bayana
mbele ya waandishi wa habari na Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Bodi
hiyo, Mhandisi Styden Rwebangila, Oktoba 31, mwaka huu mkoani Mtwara.

Rwebangila alikuwa akitoa
majumuisho ya ziara ambayo yeyé na wajumbe wa Kamati husika walifanya
mkoani Mtwara kwa muda wa siku mbili, wakiiwakilisha Bodi nzima, ambayo
ililenga kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.

Alisema, Kamati imeamua kuweka
kusudio hilo kutokana na sababu kadhaa, kubwa ikiwa ni kusuasua kwa
utekelezaji wa mradi katika maeneo ambayo mkandarasi husika amepewa
kimkataba kuyafanyia kazi huku akiwa haoneshi dhamira ya kufanya
mabadiliko chanya.

Akifafanua, alisema katika siku
ya kwanza ya ziara, Kamati iliambatana na mmoja wa wakurugenzi wa
kampuni hiyo ya ukandarasi ambapo walikagua sehemu kadhaa ambako mradi
unatekelezwa “lakini tumeshangaa leo hajaonekana katika kikao hiki
muhimu kilicholenga kujadiliana namna ya kumsaidia ili akamilishe kazi
yake vizuri.”

Alisema, kitendo cha Mkandarasi
kutoonekana kwenye kikao, kinadhihirisha kuwa hatoi kipaumbele kwa mradi
huo muhimu na wa kimkakati kwa serikali.

Akieleza zaidi kuhusu kusudio la
kufuta mkataba, Rwebangila alieleza kuwa, Kamati yake imetoa maagizo kwa
Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Huduma
za Ufundi, Mhandisi Jones Olotu, kufanya tathmini kati ya Mtwara na
sehemu ya Tanga, ambako mkandarasi husika anatekeleza mradi, wapi
panasuasua zaidi ili mkataba wake ufutwe.

Alisema, Kamati yake itawasilisha
mapendekezo ya kusudio hilo katika kikao cha Bodi na endapo
litapitishwa, utafanyika utaratibu mwingine wa kukamilisha mradi katika
eneo husika ambapo alisema Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linaweza
kupewa kazi hiyo.

Aliongeza kuwa, kusudio la kufuta
mkataba katika eneo mojawapo kati ya mawili aliyonayo mkandarasi,
haimaanishi eneo atakalokuwa amebaki nalo litatelekezwa bali Bodi na
Serikali kwa ujumla itamfuatilia kwa ukaribu mkandarasi kuhakikisha
anakamilisha kazi kikamilifu mahali patakapokuwa pamesalia ili wananchi
wapate huduma ya umeme kama ilivyokusudiwa.

Akijibu moja ya maswali kutoka
kwa waandishi wa habari kuhusu nini Bodi imejifunza katika ziara hiyo;
Mwenyekiti Rwebangila alisema “Bado tuna safari ndefu ya kuwalea
wakandarasi wazawa.”

Akifafanua, alisema, serikali
imekuwa na nia njema kuhakikisha inawapatia kazi wakandarasi wazawa
lakini asilimia kubwa, hususan wale walioungana, wanaiangusha serikali
kwani hawatekelezi miradi kwa viwango na kasi inayotakiwa.

Alitoa wito kwa wakandarasi
wazawa wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini kukumbuka kuwa wamepewa
dhamana hiyo na serikali ili wananchi wa vijijini wapate umeme na hakuna
kitakachobadilisha dhamira hiyo njema ya serikali, bali hatua stahiki
zitachukuliwa dhidi ya wale wanaokuwa vikwazo ili kuhakikisha lengo hilo
linafikiwa.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi
wa Huduma za Ufundi (REA), Mhandisi Jones Olotu, alisema Ofisi yake
imepokea maelekezo yote ya Bodi na itayatekeleza kikamilifu.

Aidha, akizungumzia suala la
utaratibu wa kisheria kuhusu kufuta mkataba wa mkandarasi, Mhandisi
Olotu alieleza kuwa hatua mbalimbali zimefuatwa ikiwemo TANESCO
kumwandikia barua za maonyo muhusika pamoja na kukaa naye vikao
mbalimbali ili ajirekebishe lakini kwa bahati mbaya hajaonesha dhamira
ya kubadilika.

“Miradi hii ni ya kimkakati kwa
serikali na sheria iko wazi. Hata hizo barua za maonyo alizoandikiwa ni
moja ya vigezo vinavyoweza kutumika kufuta mkataba,” alifafanua.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi
wake, Meneja Mradi wa Kampuni hiyo ya Ukandarasi, Mhandisi Jofrey
Luzinge, alisema atafikisha maagizo yote yaliyotolewa na Bodi kwa
Uongozi na kwamba anaamini bado wanayo nafasi ya kujirekebisha na
kukamilisha kazi husika kwa wakati na viwango, endapo watapewa ridhaa
hiyo.

Kamati hiyo imekamilisha awamu ya
kwanza ya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya umeme
vijijini, hususan katika maeneo ambako miradi inasuasua. Maeneo
yaliyotembelewa ni Tabora, Kigoma, Mwanza, Morogoro, Tanga, Kilimanjaro,
Arusha na Mtwara.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti, Kamati hiyo itakuwa na awamu nyingine ya ziara ambapo maeneo mengine mbalimbali nchini yatatembelewa.