Serikali yaahidi kutatua changamoto na kero zinazokabili viwanda vya maziwa nchini

Na Ahmed Mahmoud Arusha

Serikali imeahidi kutatua changamoto kubwa
inayokikabili kiwanda cha usindikaji wa maziwa cha Kilimanjaro fresh cha jijini
Arusha kinachokabiliwa na changamoto ya ukubwa wa kodi ya ongezeko la thamani
ambalo inabidi kushindwa kufikia uzalishaji mkubwa wa maziwa kama uhitaji wake
ulivyo mkubwa kwa jamii.

Akizungumza mara baada ya kutembelea
kiwanda cha maziwa cha Kilimanjaro Fresh jijini Arusha Naibu Waziri wa Mifugo
na Uvuvi Abdalla Ullega amesema kwamba serikali kupitia wizara yake itahakikisha
inaondoa changamoto hiyo ya tozo kwa lengo la kuimarisha uzalishaji wa
usindikaji wa maziwa katika kiwanda hicho cha Kilimanjaro fresh Milk

Ullega amesema kwamba kiwanda hicho toka
kuanzishwa kwake miezi 6 kimekua na mafanikio makubwa   “ili kupata mafanikio zaidi lazima mnunue kwa
bei kubwa zaidi kutoka kwa wafugaji ambao watapata nguvu ya kuweza kuzalisha
zaidi na kuongeza thamani ya uzalishaji wenye ubora unaohitajika,”amesema.

“Mmesema kuwa mtatoa motisha
ya mitanda endeleeni na zoezi hilo kwa kuwa ni sehemu ya kuongeza motisha kwa
wafugaji kuongeza uzalishaji kwenye bidhaa za maziwa hapa nchi nanyi kuweza
kuongeza uzalishaji wa maziwa kwenye kiwanda hicho na muendelee kufuata maagizo

Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Tanzania Abdallah Ulega akionja
maziwawyanatengenezwa na kamanda cha KILIMANJARO Fresh  wakati
alipotembelea Kiwanda hicho kuangalia namna kinavyofanya kazi(picha na
Ahmed Mahmoud,Arusha). 

Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi nchini Tanzania, Abdallah Ulega akikagua
maziwa aina ya Kilimanjaro Freshi yanayotengenezwa na kiwanda  cha 
KILIMANJARO Fresh wakati alipofanya ziara yakutembelea  kiwanda hicho
jana kilichopo Ndani ya halmashauri ya jiji la  Arusha ambapo aliwasihi
watanzania kupenda kutumia vyakwao na sio bidhaa za nje ya Nchi (picha
na Ahmed Mahmoud, Arusha)
Naibu Waziri akipata maelezo

ya serikali kwa ajili ya kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya mifugo,”.


Alisema kuwa kiujumla wameeza vizuri
katika uzalishaji wenye tija na kudai kuwa alipenda utoaji wao wa elimu kwa wafugaji katika  kuwapa elimu ya ulishaji wa chakula vizuri na kuwataka kurudia agizo la waziri mkuu kwa
kiwanda cha maziwa Asas kwenye wiki ya maziwa Kilimanjaro kuandika barua
wizarani  kuhusu malalamiko yao na wao watafanyia kazi kwa faida ya ukuaji wa tasnia

Awali akitoa maelezo ya Kiwanda hicho  mkurugenzi wa kiwanda hicho cha Kilimanjaro
Fresh  Irfhan Virjee alimweleza Naibu
waziri changamoto zinazo mkabili katika uzalishaji wa maziwa kua ni pamoja na tozo ya kodi ya VAT.

Alisema kuwa mwezi wa kwanza mwaka 2020
wanatarajia kuzalisha lita zipatazo elfu 20 ambapo pia wanatarajia kuanza kuuza
maziwa nje ya nchi ambapo walianza kuzalisha kuzalisha  lita elfu 3000 hadi sasa wanazalisha lita
800kwa siku.

Alisema kiwanda hicho kimekuwa
mkombozi kwa wafugaji  kutoka vyama vya
ushirika ambapo huwauzia maziwa kwa kiasi cha shilingi 800 hadi kufikia
shilingi 850 ambapo pia wakulima hupatiwa motisha kwa lengo la kuendelea
kutunza mifugo kwa lengo la kuboresha mifugo kupata maziwa yalio na ubora wa
hali ya juu .